Social Icons

Pages

Thursday, April 22, 2010

HAPPY BIRTH DAY HAMAD ALLY SENEDA...


Mtu unapotoka hatua moja hadi nyingine kwenye maisha kumshukuru mungu linakuwa ni jambo kheri saaana, na hii haijalishi iwe nzuri ama mbaya kwa maana tunakumbushwa kushuku mungu kwa kila jambo. Lakini kwa tulio weengi huwa twashukuru kwa mazuri tu na mabaya tunanung'unika...
Leo kwa mjukuu wa SENEDA ni raha tupu kwasababu anamshukuru mungu wake kwa kuendelea kumpa pumzi yake aendelee kuitumia bule kabisaa bila kumtoza hata shilingi 1 maana ye anasema wapo wengi waliotamani leo wawe chini ya jua lakini kwa mapenz ya mola imekuwa ni tofauti. jamaa ameongeza mwaka mmoja kati ya ile aliyokuwa nayo tangu kuzaliwa kwake....
Kuna ujumbe amenitumia kwa njia ya simu ambao si vibaya nikaunukuu hapa "kiduchu eeh, kesho siku yangu ya kuzaliwa, unajua ntaifanyaje? ntatenbea na keki kwenye gari yangu na kumpitishia kila nimkumbukae namlisha na kumpiga picha then nasepa kwa mwingine...iringa pangekuwa mbezi nawe ungekuwa mmoja wapo lazima,ha ha ha" msg imeisha jamani lol!

Mi nakutakia kila lakher katika hii siku yako muhimu mwanawane na mungu akuongezee mingi zaidi na zaidi rais wa nzese...per more jah!!!

Wednesday, April 21, 2010

ZINGATIA HAYA ILI KUCHA ZAKO ZIWE NA MVUTO.....


Inashauriwa kwamba kabla ya kuchukuwa uamuzi wa kwenda kununua vifaa husika ambayo utavitumia unapaswa kufahamu aina ya kucha ili uweze kununua vifaa vinavyoendana na kucha zako kwa lengo la kuzilinda badala ya kuvamia na kuziharibu.

Kwa kawaida kucha za mikononi na miguuni zinakabiliwa na mazingira magumu kutokana na majukumu ya kazi za kila siku hali inayochangia kuziweka katika mazingira magumu kiafya.

Mbali na kucha kukosa afya, pia kuharibu shepu yake ya awali kutokana na shughuli za kila siku katika maisha ya binadamu yeyote, hivyo ni vyema kuzikinga kucha zako na maradhi kwa kuzifanyia usafi kila siku au mara kadhaa kwa wiki ili kuzilinda zaidi.

Ili kuweza kugundua aina ya kucha zako katika kuzipangilia wakati wa kuzifanyia usafi, unapaswa kuwa makini wakati unachagua rangi ya kupaka, kuangalia muonekano wa kucha zako zilivyo ili uweze kupangalia rangi ziweze kuwa na mvuto zaidi.

Ni vyema kwa mwanamke anayejali afya ya kucha zake kuchukua muda mwingi kufuatilia kucha zake na kuelekeza nguvu zake katika kuhakikisha zinakuwa katika matunzo mazuri na kujitahidi kubuni mtindo ambao unaweza kuwa tofauti na wengine ambao wanapenda kuzifanya kawaida.

Hata hivyo, ili uwe na kucha nzuri zenye mvuto unatakiwa kunywa maji mengi kila siku ya maisha ili kupata afya ya kucha zako pamoja na mahitaji mengine mengi katika mwili wako vikiwemo vyakula vyenye vitamini nyingi.

Hata hivyo katika kutunza kucha ziwe nzuri, vyakula ambavyo ni mlo kamili ni muhimu sana, vinginevyo utajikuta ukishauriwa na wataalamu kutumia vitamini mbalimbali kama vile vitamini A, vitamini C, Culcium, Folic Asidi, Protini na Vitamini B12.

Kucha zako zitaonekana nzuri na zenye afya endapo utachukua jukumu la kuzingatia kula vyakula vyenye mlo kamili na ambavyo vitasadia katika utunzaji.....

Sunday, April 18, 2010

WERE WEREEEE! WAREREEEEE!!


Pipipipipiiiii ooooh kidedeaaa...
Wachezaji wa timu ya Simba wakiwa na kombe lao la ubingwa walilokabidhiwa jana mara baada ya kumalizika kwa mechi kati yao na watani zao Yanga katika mtanange wa kukata na shoka uliomalizika katika uwanja wa taifa wa neshno stadium.
Simba ndio mabingwa wapya wa ligi kuu ya Vodacom 2010/11

Mashabiki wa yanga na nyuso za usawajiko
maskini weeee! simba wabaya jamaniiii!? Hata hawakuwafikilia wenzao watabaki na nyuso gani baada ya kichapo? haa haa ha

Ndugu zangu wakifurahia ushindi pamoja na ubingwa pia,katika mtanange uliochezwa jana katika wanja letu la taifa la neshno stadium.

wachezaji wa yanga jamaniii...haaa haa haaaa,eti wakaanza kumzonga refa wakidai amefanya maamuzi yasiyo sahihi lol!!
(picha zote ni kwa hisani ya Mroky Mroky,Jane John na othman michuzi)

Saturday, April 17, 2010

KARIBU VITUKO.COM...


Huyu bwana aitwa ALLEN SEAN PHILLIP,ni kaka ambaye alinifanya nami nivutike kwenye hii anga ya ublogishaji.

Bwana mkubwa huyu anavituko sana kiukweli ila si vya kumkera mtu bali vyakumfanya mtu afurahi muda wote, mi ni mmoja wapo ninaezimika na vimbwanga vyake...
Mbali na yeye pia napenda saana kutembelea blog yake haswa nikiwa siko kwenye mood nzuri,maana hata kama ulikuwa hutaki kucheka hyo siku itakulazimu kukunjua ndita tu taka usitake pindi unapofungua blog yake.

Sitaki kukwambia kwanini ni lazima ucheke kwa sababu nakupa njia ya kuipata hiyo furaha ambayo mi huipata kwa kutembelea http://seanphillip.blogspot.com/ na mwisho wa siku utanijuza...

allen Sean Phillip...

Anakwambia "inawezekana kisiwa kikawa chako lakini maji akawa anayamiliki yeye" mmmh kazi ipo!!!

Wednesday, April 14, 2010

ULINZI UPO JAMANIIII???


mwenyewe upo ndani na familia yako ukiamini kuwa nje kuna ulinzi wa kutosha, kumbe hali yenyewe ndo ipo hivi....sasa wakija wale jamaa zetu(wazee wa kazi) ndo kindumbwe ndumbwe kinaanzia hapo.

Tuesday, April 13, 2010

MALIKIA WA MAWIMBI YA SAUTI...


bi shost hapa aitwa BAHATI ALEX, lakini wengi wanamtambua kwa jila la (MALIKIA WA MAWIMBI YA SAUTI) kupitia kipindi chake cha JAMBO BEAT BAABKUBWA kinachuruka kupitia ebony fm kila siku ya jumatatu - ijumaa saa 10:00 asubuhi hadi 13:00 mchana.

kuna kitu kilichokuwa kinanishangaza toka kwake sisy wangu huyu takribani miezi kadhaa iliyopita, maana tabia yake ilibadilika kidogo,mara aje ofisin kanuna,mara anachagua vyakula, wakati mwingine anasinzia tuuu...mmh! nikawa najiuliza kwani bi mkubwa huyu vipi jamani? na leo ndo kanipa jibu la swali langu.

kaniita na kunambia "haya we kiduchu nikaribishe kibalazani kwako nikupe majibu ya maswali yako" nami bila hiyana nikamwambia "karibu dada" ndo jibu likaja kuwa soon nitaitwa mamdogo...daah! nilitamani aisee kama ndo ningekuwa mie vileeee?! ha ha ha...akanambia kila jambo lina wakati wake kwahiyo wakati wangu ukifika nami nitaitwa mama.
wooow! nimeipenda hiyo bahati wangu, nakuombea kwa mola akujaalie na kila kitu kiende kama upendavyo mpendwa wangu.

kajiachiiia mwenyewe kwa raha zake...haya mama ila punguza kula chakula chenye pilipili nyingi swir..haa haa haa!!

mama mtarajiwa B-moco na sis glory....naomba uwe unakuja na mood yakunipenda mimi kila siku na kuninunulia soda kila nitakapo kama unavyofanya sasa mama,ukinichukia mwenzio ntapata tabu jamani..ha ha ha ha.

Friday, April 9, 2010

JAMANIEEEH, WIK END YAKO KUIMALIZIA NYUMBANI KWAKO SI USHAMBA...


wapendwa katika bwana,wik end ina mambo mengi saana ambayo hutokea...mazuri na mabaya,yenye faida na hasara. chamsingi ni kuwa makini ili tusiwe kwenye kundi la hasara ama mabaya mwisho wa siku. kiduchu nakutakia wik end tulivu na kumbuka kuwa kuimalizia wik end yako nyumbani na familia yako sio ushamba my....per more jah!!!

MMH! NAFAA KUWA AMA???.....


saluuuuti!!!

uso wa kikauzu lazima...ha ha ha

ntawezaaaa???

Wednesday, April 7, 2010

MADONNA....DUUH! SIO MCHEZO...


Madonna ameelekea nchini Malawi kwa ajili ya wiki nzima ya masuala mbalimbali ya hisani nchini humo.Mkali huyo wa miondoko ya pop amechukua watoto wawili katika nchi hiyo ili kuwatunza kama watoto wake na mara kwa mara amekuwa akitoa fedha nyingi katika maeneo mbalimbali na kuanzisha pia kituo maalum cha hisani na amepangiwa siku ya jumanne kuanzisha msingi kwa ajili ya ujenzi wa shule maalum ya wasichana itakayojengwa nchini humo kwa gharama zake kwa kuweka tofali la kwanza, Shule hiyo itakayojengwa kwa gharama ya paundi milioni 15 inatarajiwa kufunguliwa mwaka 2011

madonna...

KINDUMBWE NDUMBWE BADO KWA DAKTARI WA MICHAEL JACKSON...


Daktari wa Michael Jackson DR Concord Murray anatarajia kusubiri hadi june 14 wakati ambapo mashtaka juu yake kwamba aliongoza matumizi ya madawa makali kwa mwanamuziki mkali wa pop hata kusababisha kifo chake yatakapoanza kusikilizwa
Siku ya jumatatu daktari huyo akiwa katika mahakama hiyo alikutana na wapenzi na mashabiki wa mwamamuziki huyo sambamba na familia ya marehemu Michael akiwemo Janet Jackson na Jermaine Jackson wakiungana na mama yao Katherine na daktari Murray akaelezwa kuwa kesi hiyo itakuwa chini ya jaji Michael Pastor na june 14 itaana kusikilizwa
Daktari huyo amezidi kukana kuhusika na chochote kibaya kilichofanyika kwa Michael na hana kosa lolote...

michael anzi za uhai wake,akiwa na mdogo wake janet

Monday, April 5, 2010

AHADI NI DENI...MATOKEO NDO HAYA MPENDWA WANGU.


vijana wa timu ya EBONY FM wakijiandaa kwenda uwanja wa samora kung'oa nyasi katika mpambano kati yao na timu ya IRINGA SALAAM CLUB. sikwenda uwanjani kukuchukulia picha wakiwa mtanangeni kutokana na kitingwa na majukumu mengine kwa office ila matokeo niliyapata...endelea kushuka chini ukutane nayo mdau.

mwalubadu akionyesha vidole vi3 kwa maana yakumkamua binadamu 3 bila...ha ha ha japo ahadi haikutimia ila alikuwa ni m1 ya waliozitikisa nyavu za IRINGA SALAAM CLUB.

beki no 5,kaka mkuu ray na ne-mo

mnyama wao ndo alifanya kazi ya kuwapeleka vijana kazini

jamaa wakiwa wanaelekea uwanjani kwenda kumchinja mtu kama walivyoniahid...haaha haaha,na mwisho wa siku wakatoka sale ya bao mbili kwa mbili. HONGERENI SANA WOTE JAMANI (EBONY FM NA IRINGA SALAAM CLUB) per more jah saaaaana wanawane...

Sunday, April 4, 2010

NYASI ZITANG'OKA LEO SAMORA....


leo kuanzia mida ya saa 8 mchana mambo yatakuwa vizuri kunako uwanja wa samora,kutokana na burudani itakayo patikana uwanjani hapo toka wa wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya kama bi dada toka chama la tip top ZUHURA,NEMO na AWILO PETRO toka mbeya ambao watatoa burudani bila kusahau kabumbu la kung'oa nyasi toka timu ya EBONY FM na wanasalamu wa IRINGA SALAM CLUB. nimetoka uwanja wa samora sio mida kwenda kuangalia mambo ya maandalizi kuhusiana na bonanza la leo yanavyokwenda...nimependezwa na kila kinachoandaliwa hapo maana kina kwenda kama inavyo takiwa.

niko na fundi mitambo wa ebony fm ndugu ACHILEUS DESDEL ambae pia anasimamia maandalizi ya hilo jukwaa na kuhakiki kwamba kila kitu kinakuwa vyema.

watoto pia wamepewa nafasi nzuri ya kukutana na watoto wenzao leo, na ndo maana wamewekewa kitu kama hiki (bembea)

mie na golikipa wa timu ya ebony fm b-sly...nimemwambia ole wake afungishe magoli ndo atatujua si ni akina nani...ha ha ha. ntakupa matokeo mdau wangu mwisho wa siku.

Saturday, April 3, 2010

HAWA WANAKUTAKIA PASAKA NJEMA MDAU....


karafiki kangu jamani jina limenitoka....nako kanakutakia pasaka tulivu.

mie na mzee wa mishemishe j-ree...

kaka mkuu raymond na emma

JML na mwalubadu

my mdogo neema na katoto lance

eddo boy na bahati alex

allen na sisy jema

gari ya maneno HATYA OMARY

mama liner nakati ya NEMS COLLECTION, duka linalouza pamba za watu wa lika zote mtaa wa uhindini iringa tz..

b-slay,glory na j-ree

mchizi wangu GEEZY MABOVU nae kanambia nikufikishie salamu hizi....jamani tusherehekee kwa amani kufufuka kwa bwana wetu yesu kristo. amani ya bwana na iwe nawe!!

Friday, April 2, 2010

HA HA HA...DJ KWASA KAKOMESHA LEO...LOL!!


ha ha ha ha...kila aliyekuwa anakutana na sms hii hakuwa nalakusema zaidi ya kuzama mfukoni na kuchomoa mkwanja.

j-ree akisoma maujumbe kwenye mtupio wa dj kwasa...na hapa ni baada ya kupata chake.

ha ha ha,kuna watu wamepinda duniani hapa jamani lol! huyu jamaa leo kaja na mpya,kaja katupia hayo maujumbe kama yanavyosomeka kwenye kifua chake(NIMEKUJA KUSAKA HELA) kwaajiri ya kuwadai wale wooote aliokuwa anawadai. kazi aliyokuwa anaifanya ni kusimama mbele ya mdaiwa na kumwambia "soma ujumbu huu halafu zamamfukoni unirekebishie changu" ha ha ha..nikamuuliza kwanini ameamua kufanya hivyo,akasema anashangaa watu anao wadai wapo kimya tangu majuzi hawamwambii lolote wakati wanajua kabisa kuwa wanatakiwa kumlipa, sasa na yeye kumwambia mtu anaona aibu ndo maana akaona atafute mtupio wenye ujumbe wakumsaidia kuzungumza kama hivi....ha ha ha ha...aiseee nimeipenda ghafla,wewe je?
 

Sample text

Sample Text