Social Icons

Pages

Monday, July 4, 2011

UTAMU WA TIKITI....?!!


TIKITI maji linatajwa kuwa ni tunda lenye uwezo mkubwa wa kukupatia, kukuongezea vitamini na virutubisho vya aina mbalimbali mwilini.Mbali na hilo lina uwezo mkubwa wa kukupa muonekano mzuri kwa kukuondolea hali ya ukavu katika mwili na ngozi yako.Tunda hili huwa na matokeo mazuri hasa pale linapotumika kipindi cha jua kali au kiangazi.Iwapo utakuwa na utamaduni wa kula tunda hili mara kwa mara hasa kipindi cha kiangazi itakusaidia kuongeza kiasi cha maji mwilini...Yawezekana hawa chini wanakula kwakutambua faida za tikiti ama hawafahamu wao wala tu kama tunda na wengine kwa kufuata mkumbo lakini yote kwayote watakuwa wamenufaika na faida za tunda hili kwa japo leo...Karibu ufurahi nazo (Picha).

"Jamani tikiti tamu hiliii, sitamani hata liishe" Judy Mzurikwao...

"Kiduchu tunaomba kumbukumbu basi mama lol!" Juliani & Twalibu (Dr.Muwa)

"Judy mama ndo umeamua ukae karibu kabisa na mkokoteni wa bidhaa husika?"

"Mmmh! Kaka Allen lote hilo peke yako utamaliza kweli?"

"Sisy Rau unausikilizia utamu wa tikiti mama?" Jinome kwa raha zako..

Mmmmh! Julian angalia usije ukala hadi hilo ganda lol! hah hah

"We kiduchu na mwenzio Anna ndo mnasubiri mpaka Doctor awaandikie kuwa mnatakiwa mle matikiti ama ndo udadaduu unawasumbua?" Twalibu a.k.a dr.Muwa...hah hah hah huyu kaka anavituko dunia nzima hakuna laal!

Anna akaona isiwe kesi wacha nae akajumuike...

"Jamani kumbe ndo matamu hivi? Babu sijui anayatoa wapiii? Kwassa,Anna & Juddy...

Ahsante kwa kufurahi na albam hili na pia namshukuru babu matikiti kwakunipa wakati mzuri wakuchukua pia hizi bila purukushani maana wapo wengine ambao huwa hawataki upige picha biashara zao.
Nakutakia siku njema na biashara njema pia babu yangu, na kesho tena karibuuuu...

4 comments:

 

Sample text

Sample Text