Social Icons

Pages

Monday, May 21, 2012

KUTOKA MIGOLI MTERA, ZILINIVUTIA TU...Mtu na chama chake bana, bendera ya chama chako unaiweka popote unapo jisikia ili mradi pawe panapo kuhusu. Hapa ni Migoli Mtera kulikuwa na mkutano ulioendeshwa na wana chama wa CHADEMA wakishirikiana na wananchi wa Migoli kujadili kuhusu Katiba mpya.
Hawa ni marafiki zangu, nawapenda sana watoto maana ni marafiki wa kweli
Wee nani kakwambia njaa ina mwenyewe?
Hii picha niliipiga kwa mbaliii na kilichonivutia ni huyo dada upande wa kushoto alivyo chomeka chanuo kunako nywele, ni style ya zamani lakini vijijini bado wanaiendeleza sijajua kama alikuwa anataka akasuke ama ndo aliamua kuwa hivyo kwa siku hiyo. Pole mpendwa wangu picha haionekani vizuri.
Watoto bwana, ukikaa na kuwafuatilia kuanzia asubuhi mpaka jioni unaweza usiwaelewe lakini wenyewe waelewana kwa kila kitu wanachokifanya ama kuongea, mi huwa nafurahi tu na sifa na utukufu kumrudishia muumba, maana huu ni uweza wake.
Lady j dee hakukosea kutamani kuwa malaika aisee, hata mi naungana nae bana utoto raha asikwambie mtu... Kama hivi ukichafuka unaogeshwa kama bi dada Jesca hapa kwa raha zake

Bwan'kaka akipata ngoma baada ya ngoma, utamtaka sasa?

1 comment:

 

Sample text

Sample Text