Monday, July 4, 2011

UTAMU WA TIKITI....?!!


TIKITI maji linatajwa kuwa ni tunda lenye uwezo mkubwa wa kukupatia, kukuongezea vitamini na virutubisho vya aina mbalimbali mwilini.Mbali na hilo lina uwezo mkubwa wa kukupa muonekano mzuri kwa kukuondolea hali ya ukavu katika mwili na ngozi yako.Tunda hili huwa na matokeo mazuri hasa pale linapotumika kipindi cha jua kali au kiangazi.Iwapo utakuwa na utamaduni wa kula tunda hili mara kwa mara hasa kipindi cha kiangazi itakusaidia kuongeza kiasi cha maji mwilini...Yawezekana hawa chini wanakula kwakutambua faida za tikiti ama hawafahamu wao wala tu kama tunda na wengine kwa kufuata mkumbo lakini yote kwayote watakuwa wamenufaika na faida za tunda hili kwa japo leo...Karibu ufurahi nazo (Picha).

"Jamani tikiti tamu hiliii, sitamani hata liishe" Judy Mzurikwao...

"Kiduchu tunaomba kumbukumbu basi mama lol!" Juliani & Twalibu (Dr.Muwa)

"Judy mama ndo umeamua ukae karibu kabisa na mkokoteni wa bidhaa husika?"

"Mmmh! Kaka Allen lote hilo peke yako utamaliza kweli?"

"Sisy Rau unausikilizia utamu wa tikiti mama?" Jinome kwa raha zako..

Mmmmh! Julian angalia usije ukala hadi hilo ganda lol! hah hah

"We kiduchu na mwenzio Anna ndo mnasubiri mpaka Doctor awaandikie kuwa mnatakiwa mle matikiti ama ndo udadaduu unawasumbua?" Twalibu a.k.a dr.Muwa...hah hah hah huyu kaka anavituko dunia nzima hakuna laal!

Anna akaona isiwe kesi wacha nae akajumuike...

"Jamani kumbe ndo matamu hivi? Babu sijui anayatoa wapiii? Kwassa,Anna & Juddy...

Ahsante kwa kufurahi na albam hili na pia namshukuru babu matikiti kwakunipa wakati mzuri wakuchukua pia hizi bila purukushani maana wapo wengine ambao huwa hawataki upige picha biashara zao.
Nakutakia siku njema na biashara njema pia babu yangu, na kesho tena karibuuuu...

Friday, June 17, 2011

KARIBU...


Hapo vipi?

Allen Sean Phillp...
Ukiwa kwenye hiki kipindi bwana maneno yanakuwa hayana nafasi...

NILIKUTANA NAE, NIKAVUTIWA NA MTUPIO WAKE...


"Jambo jambo bwana, habari gani, nzuri sana, wageni mwakaribishwa TANZANIA yetu hakuna matata" Baada ya kukutana na huyu kaka haya mashairi yalipita kichwani mwangu hata sijui kwanini labda kutokana na hiyo jezi ama aje...mi mgeni jamani lol!!

Thursday, June 16, 2011

MMH! HII KIBOKO...!!


Kifo cha Magreth Raymond Mng'ong'o (40) kimeweza kuthibitisha kuwa dunia ni watu na kuna watu na viatu wasio penda ya watu baada ya jana usiku mume wa marehemu kujikuta katika wakati mgumu zaidi baada ya baba mkwe wake kutaka kaburi lifukuliwe na maiti kurudishwa nyumbani eneo la kitwiru ili mume huyo aweze kukamilisha kulipa mahali kabla ya mwili huo kuzikwa .Kama uonavyo jeneza lipo nje ya kaburi baada ya kufukuliwa mpaka mahali itoke ndo lirudi tena kaburini...

Mwanga wa taa za chemli na tochi ndizo zilizotumika kuongeza mwanga makaburini hapo huku mbalamwezi iliyokuwepo awali ikionekana kufifia baada ya kujitokeza hali ya kupatwa kwa mwezi na ghafla kutokea kiza katika eneo hilo.

Mazishi ya marehemu huyo yalifanyika bila ibada kama ilivyokuwa awali

Diwani wa kata ya Mvinjeni Frank Nyalusi (chadema) wa pili kulia akiwa ameongozana na ndugu wa marehemu na wananchi wakitoka kuzika majira ya saa 4 kasoro usiku

Baba mzazi wa marehemu mzee Mng'ong'o akifurahia fedha za mahali alizomtoza mkwe wake baada ya mtoto wake kufariki kwa kunywa pombe na wenzake...
Picha kwa hisani ya www.francisgodwin.blogspot.com

Thursday, June 9, 2011

BURUDIKA NAZO BASI NA WEWE...


"Mpaka mama arudi shambani ndo akoleze moto saa ngapi? Wacha mi nianze kupiliza mie"

"Kila mtu na mtue babuweee,weka pozi la picha chuchuchu"

"I u u uuuu jamani achumba uchiogope" hah hah hah

"Weee lazima nionje kabla ya wateja wangu aisee" Kitu cha ULANZI hicho, kwa huku iringa hii ndo pombe inayotutambulisha.

ITAFAHAMIKA TU KESHO HIGHLAND HALL...


Warembo watakao menyana kesho Highland hall katika kumsaka Miss Iringa..

Watoto wapo ng'aring'ari jamani lool!

Mmmh! Kazi itaonekana hiyo kesho aisee...

STEVE RNB ni moja kati ya wanamuziki wakali ambao wataupamba usiku wa kesho katika kumsaka huyo king'wasu atakae ibuka kidedea kwa kulitwaa taji la miss Iringa 2011-2012, na wanamuziki wengine watakao toa burudani ni pamoja na...

Mkali RAMA DEE....

Bila kumsahau mama lao KHADIJA KOPA ambaye ameahidi kutoa dozi kwawapenzi wa miondoko ya taarabu...

Saturday, June 4, 2011

WAPENDWA, MWANA MPOTEVU KUNDINI TENA...!!

Tuesday, January 11, 2011

BAADA YA KAZI NI BURUDANI....


Mshukuruni mungu nyie watoto, aisee wakareeeeeeeee ni noma (Hatya & Judy)

Mmmmmmh!!!

Sis Ndey...

Habari zenyu banaaaaaaaaaaa.....

Hahh hah hah hah...jamaniii loool!

Mmh! Dj kwasa, ndo kazi na dawa ama?

Shangwekeni tu vijana,wenzenu wengine wanaishia kuota tu bata kama hizi...

Duuh! Sijui mi nilikuwa wapi wajameniii??

Mamamama mamamama! We Judy weee, unamfanyia nini Allen wa watu jamaniiii? Hahh hha..

Mmmh! Glory na Mack style gani tena hiyo ya uchezaji wapendwaaa??!!

Bahati & j-ree

Jamani mpo vutooooooooooo wana da shosti (Gloy & Hatya)

JAPO NIMECHELEWA LOL!


Mzee wa mishemishe j-ree na mzaliwa (Mwalubadu)

Mwalubadu na sis ndey malisa...

Glory,Mwalubadu,Frida na mack...
Hongera sana kaka kwa hiyo miaka uliyofikisha, na mungu azidi kukupa miaka mingi zaidi. Kwaniaba ya wafanyakazi wenzangu wooooooooote twasema "happy Birth Day Mwalubadu,Mwalukokoriko,Mwalubangaladeshi na majina mengine kibao" hah hha hha hha Twakupenda saaaaaaaaaaaaana................

Friday, December 3, 2010

SIKU NYINGINE INATOKEA TU MNAJIKUTA MMEVAA NGUO RANGI MOJA...


Hatya Omary...sijui anatoa mirejesho gani jamaniii? Mmmh!

Diva J & Elly

Allen Sean Phillip

Sisy Glory

Moris , Hatya, G-Ndabagoye & Allen Sean