Social Icons

Pages

Monday, November 30, 2009

KWANI AIBU HUWA INAENDA WAPI?


teh teh teh...niko busy.

leo kuna kamjadala kalizuliwa ndani ya daladala,pale dada mmoja alipotoa nyonyo lake na kuanza kumpa mwanae ambaye alikuwa analia. konda akaanza kwa kumwangalia yule dada halafu akaguna, kuna mama akamuuliza kinachomgunisha ni nini? akaamua acheke kabisa na kusema "dada zetu bwana,hapo ndipo jeuri na maringo yenu huwa mwisho wake. leo ziwa unalitoa bila hata uoga wakati kipindi hamjapata watoto huwa mnaona aibu hata likichomoza kwa bahati mbaya"...bahati mbaya nikawa nishafika ninapoenda na kuacha kale kamjadala kanaendelea,ila kiukweli nilikazimia kweli kweli mana nami hilo swali nlikuwa najiuliza bila majibu kwamba kwa nini mtu akishakuwa na mtoto huwa huoni aibu kutoa nyonyo mbele za watu na kumnyonyesha mtoto bila aibu?...jamani wadau mi mgeni.

3 comments:

 1. Mwanzo wanakuwa wanaona aibu lakini mwisho wanazoea na aibu inaisha kabisa, hii inatoka na kujali zaidi watoto wetu

  ReplyDelete
 2. Anhaa, sasa naanza kuelewa... thanx kaka.

  ReplyDelete
 3. Kiduchu labda tujiulize kwanza kule ufukweni ambako wanaume kwa wanawake huvua nguo aibu huwa inaenda wapi?

  Maana yangu ni kwamba kila jambo hufanyika kwa wakati wake kwa maana yake, na kwa bahati nzuri ubongo wa binadamu umeumbwa kujitwist kulingana na hali na wakati,leo chuchu ileile inayofichwa na sista duu inapotolewa nje kwa dhumuni la chakula(kunyonyesha)automatically akili za watu hujitwist na kila atakayemuona hatamuona kama yuko uchi hali kadhalika na yeye mwenyewe hapo hajioni uchi. Sijui kama nimeeleweka mdogo wangu.

  ReplyDelete

 

Sample text

Sample Text