Social Icons

Pages

Friday, May 18, 2012

KILA MTU ANA MBINU ZAKE ZA USAKAJI MAHELA


Kila mtu analiwazo lake bana haswa pale anapokuwa na msongo wa mawazo, baba huyu anaekaa maeneo ya kitanzini Iringa Mjini ye liwazo lake ni hili gitaa lake, akishamaliza mishe zake za usakaji mshiko akili inakuwa imechoka kifaa pekee kinachoweza kufanya akawa sawa ni hili gitaa na analikung'uta haswaa, wanaoguswa na nikuno yake basi kumtunza hailipiwi... Mi pia ni mmoja wawalio pagawishwa nauchanaji nyuzi wake... Chukua hiyooo!!!

Wakati mzuka wa gitaa umepanda akaja mama muuza vibatari, baba huyu akamwuliza bei yake mama akasema 800, dingi huyu akasema ye anaweza kumuungisha kwa mia7, mama akasema hailipi, baba akasema ye hapo ndo anaposimamia. Kijana hapo pembeni ye alienda hapo kusikiliza nyuzi zinavyochanwa na mdingi huyu...
"Kweli babaangu siku hizi makopo ya kutengenezea vibatari hayapatikani kirahisi, kwa hiyo mia 7 hailipi chukua tu kwa 800 jamani" Mdingi akasimamia palepale kwa 700
Mwisho wa siku mama akamuuzia kwa 700
Kweli mwanaume anakula kwa jasho
Daah! Polesana kakaangu
Wauza ulanzi hawa walikuwa wanaonja kwanza ulanzi wao kabla ya kuufikisha sehemu husika...akha, raha jipe mwenyewe mwenzangu ukisubiri kupewa mbona utachachaa?!
Asikwambie mtu bwana kazi na dawa aisee, akina mama na babaz wako biz na uchambuzi wa njegere ili wateja wasipate tabu kwenye ubanjuz pembeni wapata kimiminika cha ulanzi...chukua hiyooo!!
"Sijaja kuuza sura Iringa nimekuja kusaka mahela"
"We ilete tu hata kama imeliwa na panya mi ntaipiga kiraka na itavalika tena"

Hapa genge, hapa kutengeneza majiko bora mlandi huibi cha mtu basi siku zinasonga tu...
Hapa nadhani godzilla angetafuta lakuchumpa asingekosa
Hii ndo kitanzini bana, kila mtu yupo na hekaheka zake kama hivi
Angalia kinachokufaa, toa pesa, beba halafu usepe
Wanunuzi kama kawa wakutosha
Ule mlima uliokuwa unauona kwa mbaali ndo huu upo ipogoro..

1 comment:

  1. Ag, yaani leo umenitembeza Iringa nimefurahi kweli je unaweza kupiga picha hapo ilipokuwa zamani Milimani Motel?

    ReplyDelete

 

Sample text

Sample Text