Social Icons

Pages

Tuesday, April 13, 2010

MALIKIA WA MAWIMBI YA SAUTI...


bi shost hapa aitwa BAHATI ALEX, lakini wengi wanamtambua kwa jila la (MALIKIA WA MAWIMBI YA SAUTI) kupitia kipindi chake cha JAMBO BEAT BAABKUBWA kinachuruka kupitia ebony fm kila siku ya jumatatu - ijumaa saa 10:00 asubuhi hadi 13:00 mchana.

kuna kitu kilichokuwa kinanishangaza toka kwake sisy wangu huyu takribani miezi kadhaa iliyopita, maana tabia yake ilibadilika kidogo,mara aje ofisin kanuna,mara anachagua vyakula, wakati mwingine anasinzia tuuu...mmh! nikawa najiuliza kwani bi mkubwa huyu vipi jamani? na leo ndo kanipa jibu la swali langu.

kaniita na kunambia "haya we kiduchu nikaribishe kibalazani kwako nikupe majibu ya maswali yako" nami bila hiyana nikamwambia "karibu dada" ndo jibu likaja kuwa soon nitaitwa mamdogo...daah! nilitamani aisee kama ndo ningekuwa mie vileeee?! ha ha ha...akanambia kila jambo lina wakati wake kwahiyo wakati wangu ukifika nami nitaitwa mama.
wooow! nimeipenda hiyo bahati wangu, nakuombea kwa mola akujaalie na kila kitu kiende kama upendavyo mpendwa wangu.

kajiachiiia mwenyewe kwa raha zake...haya mama ila punguza kula chakula chenye pilipili nyingi swir..haa haa haa!!

mama mtarajiwa B-moco na sis glory....naomba uwe unakuja na mood yakunipenda mimi kila siku na kuninunulia soda kila nitakapo kama unavyofanya sasa mama,ukinichukia mwenzio ntapata tabu jamani..ha ha ha ha.

1 comment:

  1. naam imetulia hiyo. nimekaribia hapa na karibu kijiweni kwangu.

    ReplyDelete

 

Sample text

Sample Text