Social Icons

Pages

Thursday, June 16, 2011

MMH! HII KIBOKO...!!


Kifo cha Magreth Raymond Mng'ong'o (40) kimeweza kuthibitisha kuwa dunia ni watu na kuna watu na viatu wasio penda ya watu baada ya jana usiku mume wa marehemu kujikuta katika wakati mgumu zaidi baada ya baba mkwe wake kutaka kaburi lifukuliwe na maiti kurudishwa nyumbani eneo la kitwiru ili mume huyo aweze kukamilisha kulipa mahali kabla ya mwili huo kuzikwa .Kama uonavyo jeneza lipo nje ya kaburi baada ya kufukuliwa mpaka mahali itoke ndo lirudi tena kaburini...

Mwanga wa taa za chemli na tochi ndizo zilizotumika kuongeza mwanga makaburini hapo huku mbalamwezi iliyokuwepo awali ikionekana kufifia baada ya kujitokeza hali ya kupatwa kwa mwezi na ghafla kutokea kiza katika eneo hilo.

Mazishi ya marehemu huyo yalifanyika bila ibada kama ilivyokuwa awali

Diwani wa kata ya Mvinjeni Frank Nyalusi (chadema) wa pili kulia akiwa ameongozana na ndugu wa marehemu na wananchi wakitoka kuzika majira ya saa 4 kasoro usiku

Baba mzazi wa marehemu mzee Mng'ong'o akifurahia fedha za mahali alizomtoza mkwe wake baada ya mtoto wake kufariki kwa kunywa pombe na wenzake...
Picha kwa hisani ya www.francisgodwin.blogspot.com

1 comment:

 

Sample text

Sample Text