Social Icons

Pages

Wednesday, March 10, 2010

KAMA WEWE HUIWEZI,WENZAKO WANAIWEZA NA WAMEIZOWEA....


huu mfereji wa maji machafu wala haupo mbali na makazi ya watu, tena pembeni tu kuna akina mama wanapika msosi (mama ntilie) na watu wanaenda na kupata msosi kama kawa bila hata wasi... nlipo wauliza wanawezaje kuihimiri hali ya harufu mbaya, walisema hiyo hali wameizowea na haiwapi tabu mmmmh! umbea wote ukaniisha nkaamua nipige picha tu na kusepa. hivi ni kweli harufu mbaya inazoeleka? mi mgeni jamani...

jamani hivi huyo mtoto anaecheza hapo kwenye maji machafu akipewa hata andazi anaweza kukumbuka kuwa atakiwa kuisafisha mikono yake ndo ale ama atalifakamia tu? na baada ya hapo kitakachofuata ninini? wazazi mnatakiwa kuwa makini na watoto wenu kwa kujua sehemu wanazoenda kucheza jamani. maana kipinduapindua hakichezi mbali kwa hali kama hyo, na washkaji zangu nao bila wasi wanastori hapo pembeni na kupunga upepo unaotoka katika beach hii hapa chini....
ajabu ni kwamba wakazi wa eneo hili hawana hata habari na hali hii,wao wanaona freshi tu ili mradi kuche.

na hawa jamaa zangu wamasai nao wana goli lao pembeni la kuwasuka akina mama na kina dada...wamenipa ofa ya kwenda kusuka ila daah! hali ya pale siiwezi wajameni.

3 comments:

 1. Yeeep Sis.
  Kuna wengine ambao ukienda walalako unaweza kujuta kama ulishasema kitu. Ndio maana nikienda kwenye makazi ya watu sitangulizi maoni.
  Ni mwendo wa kusikiliza tuuuu maana unaweza kujikuta UNADHALILISHA MAISHA YA KILA SIKU YA WATU
  Blessings

  ReplyDelete
 2. Naona unafuata nyayo za Bro.. mie,sasi sana kabinti Kaduchu.

  ReplyDelete
 3. ha ha ha...iloooh! ahsante jamani.

  ReplyDelete

 

Sample text

Sample Text