Social Icons

Pages

Sunday, February 14, 2010

ILIVYOKUWA IJUMAA NDANI CLUB V.I.P, KATI YA GEEZ NA SQEEZER..


msema chochote alikuwa mtu mzima EDDO, na hapo ndo akawa anawambia raia kuwa ule muda wa kumcheki geez na sqeezer ndo umewadia je, waungwana mpo tayariiii?

geez mabovu ndo alianza kwakukamua....

"mpo tayari watu wangu niwape mzukaaa" kelele zikasikika "ndioooo" twende sasa...

dooh! kweli shughuri ni watu na watu wenyewe ndo kama unavyowaona...

"mimi mtoto wa kiume, niacheni nijitume" haya bwana mi nnaneno hapoo? endelea tu kujituma kaka..

ha ha ha...mwalubadu na achi,kaazi kweli kweli lol!

julian,lizz one na b-slay..

jamaa alikamua ipasavyo..

baada ya mabovu kushuka,akapanda ney wa mitego ambaye alikuja kuwa kampani washkaji zake na kushuhudia wanavyo weka chuki chini na kubanjuka na mzuka wa amani..

shangwe zilimpagawisha mpaka akatoa zawadi ya shati lake kwa mashambiki...duuh! sio mchezo.

utake usitake hata kidole ungenyanyua tu kwa ule mzuka...ha ha ha

"walopanda wameshuka,wanatetemeka,jana ilikuwa zamu yao,leo ishakula kwao"...ha ha ha,aisee nduru zilikuwa za kutosha ilembaaya kwa huyu mjamaa..

yuko ok,yuko chupa,yuko maji,yuko tungi,yuko keroroooo..ha ha,haya ni mambo ya kawa saana sehemu kama hizi.

uuuuuh!

dj mubba alisimamia ipasavyo..

mzee wa anga la michezo(ibrahim issa) na mr lovenet (allen philip) wametulia tu kushuhudia kinachoendelea on da stage..

wakipagawa na mzuka wa ney wa mitego...

julian,sisy jema na kiduchu..ha ha ha,hata sijui ilikuwaje hapa..

ikafika zamu ya sqeezer kupagawisha watu wake..

mmmh! mi simo jamani...

sqeezer akichachawisha...

ha ha ha ha....utamweleza nini hapo mwalubadu na mzuka ndo umepanda?+

mashabiki wakichengeka na ngoma za sqeezer

muda wa kupatanishwa ukafika baada ya washkaji kuto kustory kwa takribani miaka 7...duuh sio mchezo na shukrani kwenu ebony enterteinment kwa kuandaa mpatanisho huu.

one love...

washkaji wakaunganisha mikono kama ishara ya kuunganisha GANGILONGA na MLANDEGE..hapo sqeezer akiwa na mchizi wa geez na geez akiwa na mshikaji wa sqeezer (dj man simple) wa kundi la jeshi wokovu...

"hamtasikia tena tuna bifu zisizokuwa na maana,sasa ni kazi tu na kaeni tayari kwa ngoma yetu ya pamoja wazeeeiya" sqeezer na mabovu

"ahsanteni saana watu wangu kwa kutuunganisha tena na mwanangu wa kitaa" sqeezer

geez,shabiki,sqeezer na achileus(fundi mitambo wa ebony fm)

jamaa wakanambia "haiwezekani lazima ung'ae nasi japo picha 1" nkaona isiwe kesi,na mambo ndo kama hivi,one love wanangu...

siunajua kihome home nini,kwahiyo jamaa anaonyesha love kwa machizi wake wa kitaa kabla ya kusepa...

No comments:

Post a Comment

 

Sample text

Sample Text