Social Icons

Pages

Friday, February 5, 2010

HIVI LENGO KUU LA KITCHEN PARTY SIKU HIZI NININI?


wandugu, kuna jambo ambalo nimekuwa nikijiuliza kwa muda mreeefu bila kupata jibu kiasi cha leo nimeamua kulileta kwenu ili nipate ufumbuzi kuhusu hili swala. Ni hivi: nimekuwa kwa kuwaona ndugu,jamaa na marafiki zangu wakifanyiwa kitchen party pale tu wanapokaribia kuolewa hata kwa yule aliyekwisha zaa mapema akiwa kwa wazazi wake, na anapofika hatua ya kubahatika kupata mchumba mpaka kufikia hatua ya kufunga ndoa nae anafanyiwa kitchen party.Sasa swali linakuja kuwa je,Huyu ambaye ana yajua mambo ya kuwa na mwanaume kiasi cha hata kuzaa zaidi ya mtoto mmoja akiwa kwa wazazi wake bila harusi…kwake kitchen party ya nini?
Na kama kwenye kitchen party swala kubwa ni kufundishwa maadili ya kumheshimu mume wake mbona wakiolewa baadhi yao hawachukui hata muda wa miaka miwili wanaachika, nap engine hata mwaka wengine hawamalizi ndoani?
Kitchen Party ni utamaduni wetu au umeigwa? Na kama ni wetu, je, hapo awali walikuwa wanafanyiwa watu ambao wakoje kitabia?....kwa maana ya “wale ambao hawakuwa wamewahi kukutana kimwili na mwanaume, yaani kutokujua lolote kuhusu mwanaume na namna ya kuishi na mwanaume ama vipi?” kama hilo ndo jibu sahihi,sasa hii kitchen party ya siku hizi lengo kubwa nini, na je ni lazima kufanyiwa hii kitu?
Wapendwa mi mgeni na hili swala,kwa hiyo karibuni kibarazani kwa kiduchu tuwekane sawa ili siku mungu akijaalia nijue kuchagua kusuka ama kunyoa……ha ha ha looh!

keki ya mafiga matatu

No comments:

Post a Comment

 

Sample text

Sample Text