Social Icons

Pages

Wednesday, February 3, 2010

HALI YA BEBE COOL INAZIDI KUWA MBAYA


Hali ya bebe cool inazidi kuwa mbaya bada ya kufanyiwa upasuaji kwa mara ya pili baada ya kuendelea kutokwa na damu katika sehemu ya mwili wake aliyopigwa risasi na askari polisi Alfred Achikan ambaye walikorofishana.
Hatua hiyo imemfanya baba yake Jaberi Bidandi Ssali ambaye ni mwanasiasa kufikiria kumpeleka hospitali jijini Nairobi kwa matibabu zaidi kutokana na hali yake kuwa mbaya inayohatarisha maisha yake.
Familia yake Bebe cool ina wasiwasi sana ambapo katika kisa hicho Bebe alipigwa risasi muda wa alfajiri akitoka kustarehe na ndugu zake waliokuwa nao kwenye gari.
Upasuaji wa kwanza ulichukua saa tano na ikiadhaniwa kwamba angepata nafuu lakini ameendelea kuvuja damu kwa wingi inayopelekea apungukiwe na damu.

No comments:

Post a Comment

 

Sample text

Sample Text