Social Icons

Pages

Thursday, February 11, 2010

BANZA STONE NA SWEET NOISE KWENYE JUKWAA 1 SIKU YA WAPENDANAO....


wenyeji wa banza (swit noise) wakiwa kwenye moja kati ya matamasha ambayo kuwakata kiu mashabiki wao huwa si kitu cha kuuliza. hawa jamaa wako vizuri sana kiukweli katika swala zima lakupiga live,na kwa kuonyesha upendo wao wameamua kumualika kaka banza kuja kufanya nao kweli siku hiyo ya wapendanao ndani ya CLUB V.I.P....kiingilio itakua ni buku 5 tu wajamani,hii haina kukosa.

mtu mzima ticha wa maticha(banza stone) atakuwepo na kupiga live na wana swit noise ndani ya CLUB V.I.P siku hiyo ya wapendanao, na couples itakayo toka chicha zaidi ya wote itapata bahati ya kwenda kulala KALENGA WEST PARK na kufanya shoping ya ajabu ndani duka kubwa mjini iringa linalouza pamba za aina zooote kuanzia mtoto mchanga mpaka mzee linaloitwa NEMS COLLECTION buuure.

DJ MUBBA KAZINI
mbali na banza stone akiwa na wenyeji swit noise,pia dj's wanaojua nini maana ya kazi yao hapa nawazungumzia dj MUBBA,KWASA,MAN SIMPLE NA MAKA watapiga disco la nguvu.

hapa ndipo wapendanao watakao vunja kabati zaidi ya woote ndo wataenda kufanya shoping ya kufa mtu buuuuure.

No comments:

Post a Comment

 

Sample text

Sample Text