Social Icons

Pages

Thursday, January 14, 2010

NYOTA NDOGO KAIGEUKIA INJILI?


muziki wa injili umeonekana kuwakamata wana afrika ya mashariki hadi inahisiwa kuwa baadhi ya wanamuziki wako tayari kusariti imani zao ili waweze kuimba muziki wa injili. mwimbaji wa gospel aliyeimba wimbo wa “jipe moyo” ametoa wimbo unaoitwa “mwachie mungu” ambao unatabiliwa kuwashika vilivyo mashabiki wa nyimbo za injili ambao pia vile vile unaweza kuzusha utata na kasheshe.
ndani ya wimbo huo wa mwachie mungu Gabriel amemshirikisha mwana muziki wa kizazi kipya nyota ndogo. Gabriel ambaye kwa siku za hivi karibuni alishaanza katika ramani ya gospel ametetea hatua yake hiyo ya kumshirikisha nyota ndogo kwenye single yake hiyo. “ nyota ni muislam na mimi ni mkristo ,lakini wote tunamtuminia mungu mmoja,ni majina tunayotumia kamtambua mungu huyo . hakuna tatizo katika kumshirikisha nyota”.kinachosubiriwa ni watu kuona kama nyota ndogo ataweza kupanda jukwaani kwenye matamsha ya nyimbo za injili kuimba wimbo huu alioshirikishwa na Gabriel,wakati yeye ni muislamu?

1 comment:

  1. Asante sana Dada
    Swali zuri na lafikirisha. Japo ni kiduchu lakini kiduchu yake yaifaa jamii
    Tusubiri majibu kwa wenye "upana wa mawazo"
    Blessings

    ReplyDelete

 

Sample text

Sample Text