Social Icons

Pages

Thursday, December 3, 2009

ETI WANDUGU,HICHO UKIONACHO HAPO CHINI NI CHAKULA AMA MATUNDA?


kuna dada mmoja leo kaniacha hoi mwenzenu kwenye kijisehem tupatacho msosi kila siku mchana. bi mkubwa aliagiza wali nyama na maharage,hakuna aliyeshangaa kwa sababu ni kitu cha kawaida. miguno ilikuja pale alipo kifuta fasta na kuagiza chipsi mayai....meza ya pili kuna kaka akumwambia "mmh dada unaonekana uko vizuri kwelikweli kiafya,na chipsi yai tena? sio mchezo" yule dada akasemaje ujue,"aliye kwambia chipsi ni chakula nani? haya si ni matunda tu kama unapomaliza kula unashushia na embe ama papai? achana na mimi wewee"..nikabaki mdomo wazi na kuwahi kuja kukuuliza mwenzangu,mana mi mgeni...

No comments:

Post a Comment

 

Sample text

Sample Text