Social Icons

Pages

Tuesday, August 3, 2010

ZIARA YA DR.SLAA IRINGA...


Kama mida ya saa5 asubuhi hivi ndo tuliingia nduli ili kumpokea
mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha (CHADEMA)Dr.Wilbrod Slaa lengo likiwa ni kutafuta wadhamini pamoja na michango kwa ajili ya kuwania nafasi hiyo (Urais)

Marafiki zangu wenyewe hawana hada mbwembwe, ilimladi kuche na giza liingie wambonji baaaaaaaasi.

Hahhah hhahh hahh...watoto hawa bwana... hah hahhh eti hapo wanacheza kishule shule.

Nikipata wawili matatu toka kwa wakazi wa nduli...kikubwa wanacholalamikia ni shida ya maji waliyonayo inayowalazimu kukaa hata siku 4 hadi 5 bila kuoga, na hali ngumu ya maisha inayosababishwa na ukame ulio kithiri pande hizo.

Mmmh! Mwenzangu hili ndo zima moto lililopo uwanja wa ndege NDULI.

mkazi wa nduli..

nikifanya mahojiano na Mwenyekiti wa mkoa (CHADEMA) Dr.Kapwani

Wanachama wa CHADEMA wakijadiliana mawili matatu..

Utani uliruhusiwa jamani...hahh hah hah.(Kiduchu & Dr. Kapwani)

Mwandishi wa makala kupitia gazeti la mwananchi sisy Tumain Msowoya na Mwanyekiti wa mkoa wa iringa (CHADEMA) Dr. Kapwani

Pipa hilooooo...kama halitaki vile.

Pipa lililo mleta Dr.Slaa lilitua uwanjani kwaraha zake..

Dr.Wilbrod Slaa alipo wasili ndani ya uwanja wa ndege (NDULI)katika ziara ya kutafuta wadhamini na michango kwa ajili kuwania nafasi ya Urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)

VIfijo na ndelemo vilitawala uwanjani pale dr.slaa alipo wasili.

Mwanasheria na mmoja wa viongozi wa ngazi ya juu katika Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)mh. Mabele Malando

Dr.slaa akihutubia mamia ya wakazi wa manispaa ya Iringa waliokuwa wamefurika katika viwanja vya mwembetogwa...Yapo mengi aliyoyazungumza, mwenye masikio kasikia na kilichobaki ni utekelezaji tu.

Wananchi wako makiiiini kumsikiliza mheshimiwa...

Kiduchu mzigoni na Dr.slaa.

No comments:

Post a Comment

 

Sample text

Sample Text