Social Icons

Pages

Monday, May 24, 2010

RENATUS KILUVIA KANIAGIZA NIKUGAWIE HII....


Asalaam aleykum ndugu zangu wapendwa,naamini mko salama kabisa,naitwa Renatus Kiluvia,ni mwandishi wa habari na mtangazaji wa redio pia,nimeandika makala hii(attachment) juu ya kipindi cha PLANET BONGO cha EATV kilivyopotosha UMMA(niaminivyo mimi) katika mfululizo wa vipindi vya wiki tatu hizi,naomba uisome kwa makini na unisaidie kuwafikishia WATANZANIA vijana hasa wapenda burudani ili waupate ukweli halisi kwa njia yoyote uonayo inafaa,iwe kuichapisha gazetini kwako au katika blog yako,nitashukuru sana,haya ni maoni yangu binafsi na wala simlazimishi yeyote kuamini.

MAKALA YENYEWE...
Wadau habari zenu,naamini hali zenu ni njema kabisa na ujenzi wa taifa unaendelea kama kawaida,leo nina mengi sana ya kuzungumza juu ya yale yaliyonikera,kama wiki tatu sasa nimekuwa karibu sana na kipindi cha PLANET BONGO cha EATV nikikifuatilia kwa ukaribu zaidi.Kwa wale wafuatiliaji wa kipindi hiki wiki hizi tatu kipindi kilikuwa kinarusha exclusive toka Mwanza(Rock City) pamoja na Arusha(A-Town).

Kutokana na hilo nimepata nafasi ya kugundua kitu, kipindi ambacho mtangazaji wa PLANET BONGO Abdalah alikitengeneza Mwanza ni wakati alipopata nafasi ya kwenda kwenye show ya mwanamuziki wa Nigeria J-Martins iliyofanyika jijini humo hivi karibuni na kile kipindi cha Arusha hakukitengeneza yeye,bali alichukuwa kipindi ambacho kilitengenezwa na mtangazaji mwingine wa kituo hicho Bhoke Egina aliyekuwa anafanya kipindi cha 5 CONNECT wakati huo na kilikwishawahi kutumika kabla ndani ya kipindi hicho cha 5 CONNECT.

Kilichonisukuma kuandika makala haya ni muendelezo ambao Abdalah aliufanya na kunitatiza,sijui idea hii aliipata wapi,napata shaka kuwa mtangazaji huyo halikuwa kusudio lake la kwanza kufanya hivyo wakati anatengenez kipindi hicho,nadhani ni idea ambayo ilikuja katikati kabisa na inawezekana ilikuja wakati tayari sehemu ya kwanza ya Mwanza na ya pili ya Arusha imeshakwenda hewani,na kilichofanyika ni ”ilimradi” kipindi cha wiki ya tatu kipatikane ili wiki ipite,hii si dalili nzuri kwa crew nzima ya kipindi pamoja na mtangazaji huyo aliyepatikana toka katika mchakato mrefu na mgumu uliohusisha vijana zaidi ya 500 waliokuwa wakiiwania nafasi hiyo mwaka juzi.

Kipindi cha PLANET BONGO cha wiki hii ya tatu kilifanywa kwa kulinganisha mikoa hii miwili iliyotumika kutengeneza vipindi vilivyopita(Mwanza na Arusha),kwamba wapi kuna muziki zaidi?Mwanza au Arusha?na wengi waliopata nafasi ya kuzungumza ni wafanyakazi wa EATV,nilipata nafasi ya kumtambua Dj Kim na maproducer wa vipindi mbalimbali vya kituo hicho,na wote walitoa tathmini kutokana na kile kilichofanywa katika vipindi vilivyopita.Yalizugumzwa mengi lakini mwisho wa siku aliyekuwa akitazama kipindi aliweza kupata matokeo japo hayakutangazwa,Arusha ilionekana INA MUZIKI zaidi ya Mwanza,chimbuko la muziki wa HIPHOP lilionekana Arusha.

Kuna mwanafalsafa mmoja alikwishawahi sema “NO RESEARCH,NO RIGHT TO SAY” akiwa na maana “BILA TAFITI,HAKUNA HAKI YA KUSEMA”,kitu ambacho crew ya kipindi cha PLANET BONGO imekifanya,crew hiyo imesema bila kufanya utafiti wa kutosha,binafsi sidhani kama hawa jamaa walikuwa na haki ya kulinganisha kimuziki mikoa hiyo miwili kwa kutumia “tuvipindi huto tuwili” walitotutengeneza.Mimi ni mwenyeji wa Mwanza,nimezaliwa Mwanza,nimekulia Mwanza,kwahiyo Mwanza naijua vizuri na muziki wa Mwanza naujua vizuri sana(hakuna anayeweza kunidanganya).

Binafsi nimekuwa mdau wa muziki Mwanza tangu napata akili za kiutu uzima,nimefanya kazi kama mtangazaji wa redio zaidi ya moja kanda ya ziwa na nimekuwa niki-deal na muziki huo kanda ya ziwa kwa zaidi ya miaka nane, ndo maana nimeamua kuzungumza haya,naamini Mwanza kuna MUZIKI zaidi ya kokote TANZANIA hii,utafiti huo nimekwisha ufanya japo si utafiti rasmi,nina utetezi na sababu nyingi na za msingi za kusema hivyo,naomba nianze kutoa utetezi wangu kwanza kutoka katika vipindi hivyo vya PLANET BONGO vilivyorushwa.

Kwanza Abdalah hakujiandaa kutengeneza kipindi rasmi cha kuja kuishindanisha Mwanza na Arusha,kitu alichokifanya ni kutengeneza kipindi cha “bora liende” ili tu mwisho wa siku ionekana hakwenda Mwanza burebure,ni dhahiri alirekodi kipindi kabla ama baada ya show ya J-Martins,kwahiyo kulikuwa na haraka ya ama kuwahi mambo mengine ya msingi zaidi yaliyomfanya aende Mwanza au kuwahi kufanya haraka ya kujiandaa na safari ya Arusha kuendelea na tour ya J-Martins ambayo kiratiba ilikuwa ipigwe siku moja baada ya show ya Mwanza,na ndio maana aliweza kuzungumza na wasanii kutoka studio moja tu ambayo ni mpya na wasanii wote ma-underground na ambao hawana hata experience ya kuzungumza na MEDIA,Dullah alizungumza na producer SAMTIMBER na baadhi ya wasanii wanaofanyakazi katika studio za A2P Records,tukianzia na hapo, A2P Records sio studio ya mfano kwa MUZIKI wa Mwanza,ni studio ndogo bado,tena sana tu,kufanyakazi na baadhi ya wasanii kutoka hapa Dar haina maana tayari imekwishakuwa studio ya mfano,wasanii toka Dar hawajaanza leo kusafiri mpaka Mwanza kurekodi. nyimbo,wameanza tangu enzi ENRICO yuko Mwanza akimiliki MWANZA RECORDS mwaka 2001

Kama Dullah alikuwa na nia ya kutengeneza kipindi Mwanza cha ushindani wa kweli angekwenda katika studio zenye muda kidogo Mwanza na kutengeneza kipindi hicho,mfano angekwenda basi MO RECORDS akaonana na producer Q ambaye sasa yuko huko baada ya kuondoka BONGO RECORDS,au angekwenda basi TETEMESHA RECORDS akapata nafasi ya kuiona studio ambayo imekwisha tengeneza HITS kibao ambazo zinachezwa kwenye redio stations kibao kila kukicha bila hata ya wapenzi wa muziki kujua kuwa kumbe nyimbo hizo zimetoka MWANZA,studio ambayo imewatoa wasanii kibao akiwemo HUSSEIN MACHOZI ambaye hakuna asiyemjua leo. Kuliko kufanya alichokifanya.

Mbali na hivyo bado huwezi kupata ripoti ya ukweli KIMUZIKI kwa kuongea na producer mmoja tena mgeni na ma-undergroung wawili watatu,historia ya muziki wa eneo fulani huwezi kuipata hivihivi tu,ni lazima uvuje jasho kwa kuwatafuta WAZAWA halisi wa eneo husika,zungumza na watu wa MEDIA wenzio wa muda mrefu eneo hilo,zungumza na wasanii wa zamani wa eneo husika,zungumza na mapromota pamoja na malegendari mbalimbali katika kiwanda cha burudani katika eneo husika utapata ripoti sahihi,kitu ambacho huyu mshkaji wetu hakufanya hata kwa asilimia moja,ndo maana napata wasiwasi kwamba inawezekana PLANET BONGO sasa inaanza kumshinda Dullah.

Vitu vyote hivyo vinahitaji maandalizi makubwa na ya muda mrefu,sio kuripuaripua,Dullah angefanya hivyo au la,angemaliza mtiririko wake kawaida bila kufanya mlinganisho KIMUZIKI kati ya Mwanza na Arusha.

Kwa waliopata nafasi ya kuzungumzia tathmini kimuziki kati ya Mwanza na Arusha katika sehemu ya tatu ya exclusive hiyo, walimtolea mfano mwanamuziki H-BABA,ni vitu vya kuchekesha sana kwakweli,H-BABA ni mwanamuziki mzuri ila sio ishara ya muziki wa Mwanza japo ametokea Mwanza,H-BABA ni “kitukuu” cha muziki huu Mwanza.

Mi nakumbuka back in a days,mwanzoni mwa miaka ya 1990 watu kama Hayati HAMAD aka TERMINATOR X(RIP),watu kama kina PAUL JAMES(PEE JAY) ambaye sasa ni mtangazaji wa Clouds na mwenzake YAQUB waliokuwa wanaunda kundi la GGV,Dj YUSUPH(yuko UK now),KASSIM MTINGWA(nduguye RUKIA MTINGWA wa VODACOM) na K-SOLO waliokuwa wanaunda kundi la WEPWAA(Wepesi Wa Akili) na makundi mengine kama III-DA FAD,II NATURE BOYS(lililomkuza FID Q) na baadae THA ROTTEN BROTHERS,BH MOBB(Toka Bugando Hill Side), G.W.A(Gangstars With Atitude),SWAHILI GENERATIONS(Toka Mlango Mmoja),CHICAGO WHITE SOX,KING KIFF NIGGA(mwandishi wa magazeti ya Sani,blogger pia),JONTWA JOKERI toka Pasiansi ambako ndo chimbuko la muziki wa Dancehall na Raggae Maffin(Ni mchungaji leo na anamiliki kanisa lake),RWEYMAN na SHIJA(RAGGEA NATION) na washkaji wengine kadha toka mikoa ya jirani kama BOB HAISA &SWEET K na jamaa flani walikuwa wanajiita PMD(PLUS MINUS DIVIDE) toka Shinyanga na wengine wengi ambao siwezi kuwataja wote hapa,hao ni baadhi ya malegendari wanaothibitisha kuwa muziki Mwanza umeanza kitambo na si juzijuzi kama inavyoonekana,wakati huo matamasha ya muziki huu yalikuwa yanafanyika GADHI HALL pale kwenye makutano ya barabara za Nyerere,Kenyatta na Makongoro,LIBERTY CINEMA mtaa wa Liberty na ukumbi wa sinema wa zamani ambao baadae ulikuja kuwa ukumbi wa disko TIVOL barabara ya Posta,baadhi ya malegendari wengine ambao hawakuwa wasanii lakini wadau wakubwa ni kama DAUDI NYALA(DAVID LATTAH) huyu ni mdogo wake na Mh.Antony Diallo,DJ ENGENEER(alikuwa MC wa matamasha karibu yote wakati huo),MARCO TIBASIMA,OSCAR MAKOYE(DJ OSCAR MARK),DJ MILIONARE(Jacob Usungu),DJ EDDY GRAND(Delux Disco),RENA CALIST(Promota),MC STOPA(Muhsein Mambo)na wengine kibao tu ambao wapo na wanaweza kupatikana kuthibitisha hilo.

Katika mtiririko wa vipindi hivyo vya PLANET BONGO wasanii wa Arusha niliwasikia wakitetea hoja yao kuwa inawezekana MUZIKI huu ulianzia Arusha hata kabla ya Dar kwa kigezo cha kwenda Arusha kwa mwanaharakati nambari moja wa BONGO FLEVA Tanzania anayejulikana kama DJ JUMANNE bila kutaja mwaka ambao jamaa huyo alitia timu Bongo hii,ukweli ni huu,JUMANNE ndio aliyefanikisha safari ya kwanza ya SUGU barani Ulaya na utengenezwaji wa albam ya nne ya msanii huyo ya NJE YA BONGO ya mwaka 1999 baada ya NIITE MR II ya mwaka 1998,sasa hiyo inaonesha wazi kuwa kama JUMANNE aliwahi sana kwenda Arusha kama wasanii wa huko wanavyodai basi haikuwa kabla ya 1995,wakati ambao tayari MUZIKI Mwanza ulikwishaanza zamani sana,na nataka niwaambie kitu kimoja wasanii wa Arusha, kuwa JUMANNE alikwenda Arusha kwa sababu za kitalii zaidi na sio kwa kuwa Tanzania hii hakukuwa na MUZIKI eneo jingine lolote.

Na awali kabisa alivutiwa na X-PLASTAZ ambao ndo BABA wa HipHop ya Arusha.Ishu ingine ni hii,mmoja kati ya mapromota wa kwanza kabisa wa MUZIKI huu Tanzania hii ni jamaa mmoja anaitwa RENA CALIST(Muandaaji Miss East Africa now),huyu jamaa ni mwenyeji wa MWANZA na suala la kuandaa matamasha alilianzia Mwanza kwa kuandaa matamasha ya “BINGWA WA RAP” Mkoa mwanzoni mwa miaka ya 1990 na baadaye mashindano kama WHOZ DA MAN yakaendelea.Kabla sijasahau MWANZA pia ni mkoa wa pili kuwa na redio station baada ya Dar(Radio Free Africa) ambayo ilianza mwaka 1995 mwishoni,kwahiyo ni moja kati ya vitu vikubwa vilivyochangia maendeleo ya muziki huu ambao tayari ulikuwepo.

Shahidi mwingine ni aliyekuwa mtangazaji wa Radio One wakati huo ambaye aliacha kazi pale kwa harakati hizihizi za kuutambulisha muziki huu na kuhamia RFA mwaka 1996 TAJI LIUNDI(MASTER T),huyu alikuta MUZIKI uko tayari MWANZA na vijana wameaanza kurekodi japo kwa studio zilizokuwa chini ya kiwango.

Nina mengi sana ya kuzungumza jamani juu ya utetezi wa point yangu kuwa si kweli kwamba Arusha ndio chimbuko na ndo kuna muziki zaidi ya Mwanza.

Mwanza kuna kila kitu leo kinachoweza kuupeleka muziki mbele zaidi,Radio kubwa kuliko zote katika nchi za Maziwa Makuu iko Mwanza na pia ndio redio pekee yenye usikivu mkubwa Tanzania nzima(RADIO FREE AFRICA),TV station kubwa yenye wigo mpana TANZANIA pia iko Mwanza(STAR TV),watangazaji wanaoijua kazi na wenye hamasa na moyo wa kuutangaza muziki wa Mwanza pia wako kibao kule,hata hao wasanii wa Arusha wanaodai kuwa Arusha ndio kuna muziki zaidi kuliko Mwanza wanategemea promo kutoka kwa watangazaji na media hizo,sasa iweje leo Mwanza iwe chini??Kikubwa nnachoweza kuwashauri wasanii wa Mwanza wa leo,wasilewe na vijisifasifa wanavyovipata kwa airtime ndogo wanayoipata toka katika viredio vidogo vidogo vya hapo mjini,wajitume na watumie rasilimali iliyomo jijini humo kuufanya muziki wao uwe juu zaidi,washirikiane na wadau wa muziki jijini humo,waige mifano ya malegendari waliopita na wakubali ushauri toka kwetu sisi kaka zao,waache uadui usiokuwa na tija na watangazaji wa redio za hapo mjini,zaidi watengeneze NETWORK ili waweze kujitangaza kimataifa na sio kuridhika na tusifasifa wa kijinga.

My last point but not list japo ninazo zingine nyingi,kama nilivyoeleza katika aya ya kwanza ya makala hii,kuwa kipindi ambacho kilirekodiwa Arusha si kipindi ambacho kilitengenezwa jana wala juzi,ni kipindi cha muda mrefu kidogo na kilitengenezwa na mtangazaji wa kipindi cha 5 CONNECT wakati EATV imeanza kuonekana Arusha na Moshi kama karibu kwa wakazi wa mikoa hiyo,hivyo nachelea kusema kuwa kipindi cha Arusha kilikuwa kimeandaliwa na kilifanyika kwa kutafuta wanaojua kuzungumza na MEDIA na wanaoujua MUZIKI wa Arusha vizuri tofauti na kipindi kilichotengenezwa Mwanza.

Nadhani ndio maana Arusha ilionekana kuna MUZIKI zaidi kuliko Mwanza kitu ambacho nina uhakika si kweli.Jamani haya ni mawazo yangu tu mimi binafsi na wala yasimkwaze yeyote atakayesoma makala haya,ila naomba watangazaji na waandaaji wa vipindi mbalimbali vya redio na Tv wafanye tafiti za kutosha kabla na baada ya kutengeneza vipindi vyao na kabla ya kuvipeleka hewani,hii itapunguza kama si kuondosha kabisa mkangayiko na jamii kupelekewa taarifa zisizo sahihi juu ya mambo mbalimbali.Akhsante kwa kusoma mwanzo mpaka mwisho makala haya na kama una mchango,maoni au ushauri basi wasiliana nami kwa email zifuatazo bizzo4shizzo@ymail.com au renatuskiluvia@ymail.com .
AKHSANTE na KAZI NJEMA.
Wako katika ujenzi wa taifa...
Renatus aka Bizzo.(0655-260083)
NB;Pia Makala haya yanapatikana katika blog yangu www.muzikinamaisha.blogspot.com.

No comments:

Post a Comment

 

Sample text

Sample Text