Social Icons

Pages

Wednesday, January 20, 2010

"MIMI SIO MLOKOLE"- NYOTA NDOGO


Baada ya watu lukuki kushangazwa na kitendo cha mwanamuziki nyota ndogo kuimba na mwana gospel Gabriel anae hangaikia kutoka tena kwenye chati ya muziki wa injili nchini Kenya,nyota mwenyewe ameibuka na kuweka kila kitu hadharani. Nyota ndogo amekanusha kutaka kubadiri dini na kuwa mkristo na kukanusha uvumi kuwa amekuwa mlokole..”mimi sijaokoka bado ni muislam, nilichokifanya nikuimba wimbo na mwimbaji wa gospel ,na nimefanya hivyo kwa mapenzi yangu kwa mungu na si vinginevyo” amesema nyota.wimbo wa “mwachie mungu” kwa madai ya waliokuwepo wakati wimbo unarekodiwa wamesema kuwa nyota alikubali kuimba baada ya kuyakagua mashairi ya wimbo woote na kuona hakuna sehemu yenye jina la yesu ndipo akaingiza sauti.

No comments:

Post a Comment

 

Sample text

Sample Text