Monday, January 25, 2010
KAZI KWETU WALA UYOGA...
Uyoga unaojiotea hovyo huu haufai kuliwa kwasababu inasemekana unaweza kuwa ni sumu kwani Uyoga huo unaojiotea hovyo, Huota sehemu chafu kama katika sehemu za mkusanyiko wa maji maji, Maji yale yanapokuwa yanakaa muda mrefu katika sehemu ile huzaa wadudu na kufanya utelezi fulani na baada ya muda hutokea huo Uyonga ambao unasemekana ni sumu
kuna uyoga wa kupandwa na uyoga unaojiotea wenyewe bila kupandwa. Uyoga wa kupandwa unatakiwa uwe umepandwa katika sehemu yenye usafi ambayo haitaweza kumuathiri mtumiaji anae taka kuutumia kwa kuula...
Uyoga unaoliwa huimairisha kinga ya mwili na ni chakula kinachoupatia mwili protini pia. Tunaweza kupika uyoga kama mboga au kuutumia katika saladi, sosi au kuuchanganya katika vyakula vinginevyo kama vile pizza n.k....picha kwa hisani ya kaka mjengwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Yaani we acha tu, nimeutamani uyoga huo na pia nimetamani nyumbani maana hapa itabidi nisubiri mpaka wakati wa summer duh!
ReplyDelete