Social Icons

Pages

Friday, December 18, 2009

MMH! KAAAZI KWELI KWELI MWAKA 2009 KWA WANAMUZIKI WA AFRIKA MASHARIKI....


Wakati nonini alipotoka na singo yake yenye kibwagizo chenye neno “kadhaa” ilikuwa imebaki miezi kadhaa,wiki kadhaa,siku kadhaa,dakika kadhaa na sekunde kadhaa ili kuumaliza huu mwaka 2009.

2009,ni mwaka unaosemwa kujaa timbwili timbwili za kila aina zikiongozana na matamasha kibao ya kimataifa na ni mwaka ulioshuhudia wasanii lukuki chipukizi wakiibuka na kutishia uwepo wa wasanii maarufu wa afrika mashariki.

East Africa imebarikiwa kizazi kipya cha wana muziki na watunzi wa mistari iliyo simama, lakini pia ukanda huu umegandwa na laana na mikosi kibao kuanzia mabosi ambao wamekuwa wakiwanyonya wasanii haki zao hadi bifu miongoni mwa wasanii wenyewe.

Mkali wa kuingiza vocal kwenye ngoma za bongo RASHID MAKWILO ama chid benz anachukuliwa kama ndiye mwanamziki mgomvi kuliko wote kwenye bongo fleva kwa mwaka huu ambapo ubabe wake ulianzia kwa matonya kabla ya kumpa nakoz na kummalizia kaka mkubwa profesa jay.

Wakati chidi akiwatikisa wenzie kwa masumbwi hapa bongo,huko uganga mtikisiko wa uchumi ulimlazimisha manager wa kundi la obsession na kulazimika kuwatema wanamuziki wawili wa kundi hilo na kubakisha wanamuziki wa3.

Kama gundu vile kwa wanamuziki wa Uganda , nae raisi wa ghetto bob wine alipata hasara za mamilioni baada ya moto kuteketeza mali zake . wakati balaa hilo likitokea mtu mzima bobi alikuwa busy ana-promoti albamu yake iitwayo “Carolina” …swali ni je,2010 itakuwaje? kama2009? Ama hii itabaki kama story?

No comments:

Post a Comment

 

Sample text

Sample Text