Social Icons

Pages

Wednesday, November 11, 2009

MSIMU WA MAEMBE NDO HUOOOO...


wandugu,msimu wa maembe umesha ingia mana kila kona utakayo katisha si kitu cha kushangaza kukutana na wauza maembe zaidi hata ya watatu kwa huku kwetu sijui kwako we mwenzangu. sasa swala kubwa hapa ni kuwa makini sana na usafi maana kama tujuavyo msimu huu huambatana na inzi weeengi,na jamaa hawa huleta magonjwa mengi haswa ki pindupindu kwahiyo usafi kabla ya kulila hlo embe lako na mahali husika wahitajika....POROJO...nasikia ukitaka kuharibu shughuri ya watu kama kuna matarumbeta, we jipitishe tu kwa madoido na embe lako huku ukilila taratiiiibu kama akina bidada hapo uone wapiga matarumbeta wanavyovuruga utaratibu....teh teh teh.

No comments:

Post a Comment

 

Sample text

Sample Text