Saturday, November 21, 2009
MAMBO YOTE KALENGAAAA........
UMBALI wa kilometa 16 kutoka Iringa mjini ndipo kilipo Kijiji cha Kalenga, ambacho kwa wanahistoria si jina geni kwao, kutokana na umaarufu wake katika harakati za mapambano dhidi ya ukoloni.
hizo ni siraha walizokuwa wakitumia kupambana na mahasimu wao
hili ni box lililobebea fuvu la chifu mkwawa toka ujerumani kuja Tz
weeee, iba fuvu la chifu nikufyatulie.
nikiwa na mwandishi wa makala wa gazeti la mwananchi dada tumaini msowoya ambaye tulienda wote kalenga.
huyu ndo chifu mkwawa ambaye historia yake ya ushujaa ilinaanza rasmi mwaka 1874, akiwa na umri wa miaka 19 alipopewa uchifu na baba yake anayeitwa Munyigumba ambaye ndiye alikuwa chifu wa kwanza wa Uhehe.
hili ni fuvu la chifu mkwawa lililorejeshwa Tanzania toka Ujerumani Juni 19, 1954, ikiwa ni miaka 56 tangu siku aliyojiua.
nikipewa mawili matatu na mpokea wageni ndugu Nicholaus Mkulanga.
nikiwa nje ya nyumba ya makumbusho inayo hifadhi fuvu la chifu wa wahehe, Mkwawa Mkwavinyika Munyigumba Mwamuyinga aliye zaliwa mwaka 1855 na kujiua kwa kujipiga risasi mnamo mwaka 1898.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Ahsante kwa historia hii nzuri.Ni kumbukumbu nzuri.
ReplyDeleteahsante pia mpendwa.
ReplyDelete