Wednesday, November 4, 2009
GARI YA MANENO HIYOOOO....
aitwa hatya omary hilo ndilo lililopo kwenye cheti chake cha kuzaliwa. majina ya njaa sasa...mama sinyorita,mwarabu wa dabaga,gari ya maneno na mengine mengi niki yaorodhesha hapa ntachelewa kurudi nyumbani buuure,hayo kiduuchu yakutosha.
bi mkubwa huyu leo aliniacha hoi sana kwenye segment yake ya "vijimambo" ndani ya kipindi cha JAMBO BEAT BAABU KUBWA akiwa na BAHATI ALEX. ambapo leo kaja na kijimambo kinachoendelea kwa dada mmoja anaependa kupigwa na mumewe kila siku, unaambiwa kama siku hiyo akiona mumewe hana mpango wa kumpiga basi bibie atafanya kila liwezekanalo ilimradi akazifichue hasira za mumewe zilipo ili apate kidundo....ha ha ha,wakati wengine twaogopa hata kupigwa kofi kumbe wenzetu wengine wapenda,,,,eti kupigwa ni kuongeza chachandu ya malavdaviiii....ha ha ha ama kwahakika ni vijimambo....
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
majina ya njaa:-)
ReplyDeletendo maana yake kaka...
ReplyDelete