Social Icons

Pages

Thursday, October 29, 2009

USIPOTEZE PESA YAKO WAKATI DAWA NI BUUURE..


KIKWAPA kusema ule ukweli ni tatizo linalo wakosesha amani watu wanao wasumbuliwa na tatizo hilo, kuna dada mmoja ambaye ana hili tatizo kanambia kwamba imefika kipindi yeye anaamua kujifungia ndani kwake kwa kuogopa kukaa na mashostito wake halafu akaharibu hali ya hewa. nimejisikia vibaya na nikamwahidi kumtafutia ufumbuzi kwa niaba ya wengine wenye tatizo kama lake pia. japo wengi wamekuwa wakitumia sabuni, krimu na hata pafyumu za aina mbalimbali kwa ajili ya kuondoa uchafu wa kwenye kwapa lakini bila ya mafanikio yoyote.

HIZI NJIA ZAWEZA KOKOMESHA HILI TATIZO:
-Usafi inaweza kukusaidia.
-Malimao na ndimu ni vitu vyenye uwezo mkubwa wa kuondoa harufu na uchafu katika kwapa.
-Matumizi ya ndimu na limao yana matokeo mazuri kwamwili wako kama utatumia kikamilifu.
-Unachotakiwa na kufutafuta limao au ndimu unaikata kisha unakamua.
-Chukua kitambaa weka maji maji ya limao na kisha anza kusugua taratibu kwapa lako.
-Hakikisha unafanya hivyo wakati ukiwa umetoka kuoga.
-Pia unaweza kukata limao au ndimu bila ya kukamua na kuanza kusugua katika kwapa lako.
-Vitu hivyo vina nguvu za kuondoa uchafu katika kwapa.
-Ni muhimu kusafisha kwapa kwani kwapa linapokuwa si safi hata unapovaa nguo ya wazi unakuwa huna uhuru wa kunyanyua mkono juu pindi inapokulazimu kufanya hivyo.
Kwapa ni sehemu muhimu sana ni lazima iangaliwe kwa namna ya pekee na uhakikishe unakuwa safi muda wote ili kuondoa harufu na muonekano mbaya katika kwapa....Haya jamani nimekupa kiuduuuchu lakini nikiwa na imani kuwa umetosheka,jaribu unipe matokeo,,,,,

No comments:

Post a Comment

 

Sample text

Sample Text