Wednesday, October 28, 2009
NYOTA NDOGO ATOKA NA TAY GIN
nyota ndogo mwanadada maarufu kutoka Mombasa nchini Kenya,aliyetoka na single nyingi 2 zilizo mfanya mpaka sasa azidi kung’ara kwenye game hii,ameamua kutanua mbawa zake kimuziki hadi nchini Malawi kwa kurecod wimbo na raper mashuhuri nchini Malawi TAY GIN. Goma hilo linalo kwenda kwa jina la “AM GONNA BE FINE”ni kama vile mtihani kwa nyota ndogo kwani kwa siku kadhaa amekuwa akipiga buku ili kuongeza uwezo wake katika lugha ya kiingereza. Uwezo wake wa kuflow na sauti yake nzuri umenshangaza kila mtu, single hiyo iliyo rekodiwa miezi miwili iliyopita mjini Mombasa ndani ya studio za G-Rec,Tay Gin ameshikirikishwa mara tu alipokuwa mjini Mombasa kwa mapumziko binafsi.Nyota ndogo mwanamziki mkenya anaye miliki bend,alianza muziki wake akitokea kwenye U-HOUSE GARL ,nyota ameitabiria ngoma yake hiyo kufanya vizuri kwa soko zima la mziki kwa Kenya na afrika mashariki kwa ujumla.Nyota ndogo pia ametengeneza wimbo mwingine na DJ Mapunda wa channel O. Tay Gin hivi karibuni alizindua albam yake ya pili nchini Malawi ambapo mwanamziki nguli wa Kenya asiye na jina (NAMELESS) alikuwa mwanamziki mwalikwa aliyeitwa kuperform.
Tay gin tayari amesha perform kwenye shindano linaloendelea la BIG BROTHER AFRICA REVOLUTION mara mbili na ameteuliwa kushindania tuzo za channel O za video kali za muziki kwa mwaka wa tatu mfululizo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment