Social Icons

Pages

Friday, September 3, 2010

KIPI MUHIMU KATI YA ELIMU YA MSINGI NA SEKONDARI?


Baaada ya seriklai kuamua kuhamasisha ujenzi wa shule za sekondari za kata na kufanikiwa kwa kiwango cha juu,Ebony Fm kwa ushirikiano na Tanzania Media Fund TMF imeamua kuanza kufuatilia kwa undani na ukaribu maendeleo ya shule za msingi ili kulinganisha na juhudi katika ujenzi wa shule za sekondari za kata katika mikoa ya nyanda za juu kusini.
Hakuna ubishi kwamba ili shule za sekondari za kata zipate wanafunzi nguli na wakujivunia sharti shule za msingi kote nchini ziangaliwe kwa macho yote mawili na siyo vinginevyo.
Lakini hali imekua tofauti kabisa ambapo katika shule ya msingi wanging’ombe wazazi wamehamasika sana na kuamua kujenga shule ya sekondari wanging`ombe na kuitelekeza shule ya msingi wanging`ombe.

SHule ya msingi wanging`ombe ilijengwa mwaka 1946 chini ya rais wa kwanza wa jamhuri ya muungano wa Tanzania hayati baba wa taifa Mwalimu Julius K.Nyerere na kuwekwa jiwe na yeye mwenyewe mwaka 1964.

Kama hiyo haitoshi shule hii hata kama imetelekezwa bado ukweli wa mambo utabaki palepale kuwa kuna viongozi wengi sana ambao wamesoma katika shule hii ya msingi wanging`ombe akiwemo Katibu mkuu kiongozi Fillmon Luhanjo

Inasadikika kuwa katibu mkuu huyo kiongozi amewahi kufika katika shule hiyo na kuahidi ahadi lukuki ambazo hadi Ebony Fm inaondoa katika eneo hilo hakukua na taarifa zozote juu ya utekelezaji wa ahadi hizo.
Miongoni mwa ahadi hizo ni pamoja na saaruji,nondo kwa ajili ya ukarabati wa madarasa ya watoto wa awali na darasa la kwanza.

Kwa upande wake mkuu wa shule hiyo mwl. ZARIAN GUNTROM NGALIOMA ameulaum ungozi wa serikali ya kijiji hicho kuigeuzia mgongo shule hiyo huku uongozi huo ukimiliki mali za shule kama vile ng`ombe.
Kwa mujibu wa mwalim mkuu huyo ng`ombe hao waliletwa na mwalim JK Nyere enzi za uhai wake kama mradi wa maendeleo ya shule hiyo ya msingi lakini serikali ya kijiji ikaamua kutaifisha.

Afisa mtendaji bwana MEDSON NGELA alipotakiwa kujibu tuhuma hizo za kutotoa ushirikiano wa kimaendeleo katika shule hiyo amesema siyo kweli kuwa serikali yake ya kijiji imetelekeza shule hiyo ya msingi.
Kama hiyo haitoshi serikali imefanikiwa kwa kiwango kikubwa hali ambayo imewapotezea wananchi imani ya kuamini kuwa mwanzo wa sekondari unatokana na msingi mzuri wa shule hizo zinazojulikana kama shule za msingi a.k.a mfereji.

Hii ni picha ya majengo ya shule ya sekondari Wanging`ombe mita chache tu kutoka shule ya msingi wanging`ombe.

Na hii ni picha ya moja kati ya majengo ya shule ya msingi wanging'ombe ambako kimsingi ndiyo mtoto anatengenezwa tayari kwaajiri ya kujiunga na elimu ya sekondari...
Jeee, kwa mtindo huu wapi tunakosea? au tuko sawaaa? Jamani mimi mgeni katika hili.

Picha hii ni jengo lachoo cha walimu cha zamani enzizileee za akina LUHANJO wakati anaisaka elimu ya msingi wanging'ombe.

Kwa ndani muonekano wake ndo upo hivi..

Nahii sasa ndo up to date teacher's toilet sijui kama nimepatia,ila namaanisha "ndo choo mpya ya walimu kwa sasa"

Mwandishi wa ebony fm (Raymonnd)a.k.a kaka mkuu akifanya mahojiano na wananchi wa wilaya mpya ya wanging'ombe mkoani njombe, juu ya mstakabali wa shule hiyo.

Mzuka wawananchi ukazidi kupanda juu ya hatma ya shule yao, maana pamoja na kutoa michango yao kama wazazi ili kunusuru hali iliyopo lakini wanashangaa hali bado ni duni.

Hawa ni wanafunzi wetu wa shule ya msingi wanging'ombe,ambao ambao matarajio ya wengi ni kufika katika elimu ya juu...Sasaa, kwa mtaji huu wa kusafisha kikombe nje na kusahau ndani jee,elimu bora inawezekana ama bora elimuuuuu? M
simooo....Ahsante TMF,ahsante EBONY FM....

No comments:

Post a Comment

 

Sample text

Sample Text