Social Icons

Pages

Friday, May 21, 2010

BELLE9 NA DIAMOND KUUSUUZA USIKU WA KUMSAKA MISS IRINGA LEO....


Belle9 na Diamond ndo wasanii watakaotoa burudani ya kusindikiza shindano la kumsaka miss iringa 2010 leo usiku ndani ya ukumbi wa St.Dominic.

Belle na Eddo(Mratibu wa miss iringa)

B-sly na Belle9

"Tatizo kwetu mbagala haa,hapa nyumba mbele jalala haa,tatizo kwetu mbagala,ukaniona mapenzi siwezi" mmh..kaaazi kweli kweli.

"Uko mbali na masogangee,njoo utulize mtima wanguee,mapenzi yanautesa moyoweee,mapenzi yanaumiza moyo" ha ha haa...mi simoooo!!

Belle,B-sly,Diamond na Eddo

"Wakazi wa iringa hawatojuta kwa kiingilio watakacho dondosha mlangoni leo" Maneno ya belle na Diamond hayo...

Nami sikuona kama ni dhambi kuonyesha mapendo kwa njia ya picha kama hivi na vijana hawa wajameni.

Belle anavituko sana...kuna vijiutani alikuwa anamtania Diamond hapo kila mtu alinyoosha mbavu kiukweli.
Safi saaana aisee,nimewapenda zaidi ya mwanzo hawa madogo kiukweli.

Baada ya kushow mapendo,mwendo kuelekea sehemu walofikia (HOTELIN) kujipumzisha kiaina ili wakiingia mzigoni baadae mwendo uwe mmoja tu,wakutoa burudani ya uhakika.

"Mzuka basi dada kiduchu,si wacha tukapumzike kidogo...tutakutana st.dominic hiyo badae kama vipi" Belle9 na diamond.
Nami nikawambia "pouwa pouwa wadogo zangu"

No comments:

Post a Comment

 

Sample text

Sample Text