Social Icons

Pages

Monday, February 22, 2010

ANKO HINDI LAKO LIPO TAYARI NJOO...


Jana nlikuwa na mshkaji wangu dj mubba mida ya jioni hivi wakati tunatoka job, nikawatamani mahindi ya kuchoma baada yakuyaona kwa mbaali,mubba akasema twende tukanunue. si ndo tukafika sehemu husika na kukutana na bwana mdogo huyu. nikamwuliza alipo muuzaji mahindi kwa sababu sikufikiria kabisaa kwamba hilo goli atakuwa analisimamia yeye, bwanawee...dogo akanambia yeye ndo muuzaji na ile biashara ni yake kwahiyo nichague tu hindi linalo nifaa..lol! nikamuliza kama anasoma,akasema ndio anasoma na jioni ndo huwa anakuwa kwenye uwajibikaji wa kusaka riziki kama nimwonavyo. Nilishangaa pale aliponiomba simu ili ampigie mteja wake kuwa hindi alilo mwomba amchomee lipo tayari, nikamwuliza tena kuwa inamaana ananamba hadi za wateja wake? akasema ndio na hata kama na mimi nataka nimwachie no yangu atakuwa akinipigia kama nataka mahindi ila muda ule simu yake ilikuwa imeiha salio eti hata la kubip... ha ha ha dogo huyu bwana! ikabidi nimpe kimeo changu na mambo ndo kama uyaonavyo..

No comments:

Post a Comment

 

Sample text

Sample Text