Thursday, November 5, 2009
MTOTO UMLEAVYO,NDIVYO AKUAVYO...UONGO?
Wazazi na walezi wanaweza kuwa na nafasi kuu na muhimu katika makuzi na usafi wa mtoto, masuala ambayo atakuwa nayo katika maisha yake ya kila siku. Kitendo cha kumfunza mtoto kuhusu usafi wa mwili ni njia bora kabisa ya kumuepusha na maambukizo na maradhi mbalimbali. Ni jukumu la mzazi au mlezi kumfunza mtoto misingi sahihi ya usafi wa mwili wakati mtoto akiwa na umri mdogo kabisa, jambo ambalo litamsaidia mtoto huyo na familia yake katika maisha yao ya baadaye.
bi dada kwa raha zake anafua....ha ha ha. kazana mwayego
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Safi sana nimefurahi kuona taswira hizo. Ni kweli mtoto umleavyo ndivyo akuavyo. Nayapenda maisha hayo ya kuwafunza watoto tangu wapo wadogo.
ReplyDelete:-)
ReplyDeleteTukumbushe kuendelea kuwalea namna tufanyavyo wakiwa wadogo. Tukiachia niani watajitahidi kurejea mpaka yale waliyokuwa wana-miss na ndio maana wanaharibikiwa. Si mnaona watoto wa WATUMISHI WA MAKANISA???
ReplyDeleteBlessings