Wednesday, September 29, 2010
ENZI ZETU AKINA SIE BANA....HAHH HAHH HAH!
Kilakitu kinakwenda na kubadilika kila kukicha, miaka ya nyuma kidogo kalamu na karatasi vilikuwa ni vitu muhimu saaaana katika swala zima la kurusha ndoano yako kwa mtu anaeutesa mtima wako na ungependa awe kimwali wako ama mwandani wako,hahh hahh hahh....
Lakini siku hizi, aah mambo ni bwelele kabisa ni kitendo cha kupata no yake na kumwendea kwa hewa halafu mtu mzima unamwaga sela zako, akikuelewa pouwa akidengua unapotezea...hahh hahh.
Ila mwenzenu mi naimiss kwelikweli njia ya zamani maana mtoto wa kike ulikuwa lazima uweke mashebeduzi kwanza ndo kama nawe umempenda jibu anakuja kulipata baadae kabisa.
Vipi we mwenzangu njia ipi pouwa sana kwako, kati ya yazamani ni hii mupyaaaaaaaaa???!!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Hapo kuna kitu umesahau.
ReplyDeleteIlikuwa unatengeneza "V" kwa vidole (kama ileee ya alama ya PEACE) kisha unaweka kwenye ulimi na kugandamiza kwenye karatasi. Basi maandishi yanaonekana kama yamedondokewa na maji, halafu wamwaga sera kuwa "hapa niandikavyo machozi yananidondoka, unaona nimeharibu hata barua yako mpenzi"
Hahahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
Siasa zilianza zamani jamani. Enzi za kuota bila kulala na kutokunywa maji maana wamuona kwenye glasi na hukati kitunguu maana wahisi mwamkata yeye?
Mmhhhhhhhhhhhhhh
SWALI.......Huu ni mwandiko wako Aggie. Ulimuandikia nani????
Hahh ahhh hahh hah..sina neno mieeeeeeeeeee yoote umeyamaliza weye Mzee wa Changamoto...hah hhha hhah
ReplyDelete