Mie kwa mtazamo wangu mume mwema ana sifa zifuatazo kwa uduuuchu,japo zipo sifa nyingine nyingi:-
1. Ametulia si macho juu juu kama nzi kila akionacho hata kichafu chaliwa.
2. Anajiheshimu,anamuheshimu mkewe, ndugu wa pande zote, watu wengine pamoja na majirani pia.
3. Mwenye huruma na mapenzi ya kweli kwa mke na familia kwa ujumla.
4. Mtunzaji wa familia na si bahili au mfujaji wa mali.
5. Mcha mungu, au mwenye utu.
6. Mchapa kazi,asiye kata tamaa, si mvivu na goi goi
7. Msaidizi, sio mke na jembe na kuni yeye kashika bakora anapunga mkono, shughuli zote za uzalishaji mali na utunzaji familia kamuachia mke.
8.Mwenye kupenda kujadiliana, sio amri ikitoka imetoka hata kama pumba zenye madhara mradi yeye kasema basi naibaki kuwa hivyo.
9. Mwenye kutimiza wajibu wake kwenye masuala ya unyumba, sio mume jina, "chakula" anakula barabarai mkewe anabaki na "njaa"…ha ha ha lool!!
10. Mwenye kuona wivu kwa mkewe sio kila mtu basi ruhsa kula "chakula" nyumbani kwake ilimradi yeye kaoa basi kaolea jamaa na marafiki.
Na nyingi nyinginezo ndio zinatengeneza sifa za mume mwema, ametoka wapi kijijini au mjini hiyo sio ishu sana.
Friday, May 28, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
DUH!!!SASA MBONA MI NINAZO ZOTE JAMANI???ILA KASORO MOJA TU,YAAAAAAAAA......NGAPI VILE??HEBU NGOJA NICHEKI VZR..
ReplyDelete