Social Icons

Pages

Featured Posts

Wednesday, July 16, 2014

NI WEWE KAMPENI, MAENEO YA ITUNUNDU PAWAGA JANANi Wewe ni kampeni iliyozinduliwa na redio Ebony FM iliyoko Nyanda za juu kusini, ikiwalenga zaidi wananchi wa vijijini ambao miundo mbinu ya umeme bado haijawafikia kwakuwasaidia kwa kuwapa majokofu yasiyotumia umeme, unga wa ngano na nguo... Hii yote ikiwa na dhumuni kubwa la kurudisha fadhila kwa wasikilizaji wa redio Ebony FM kwa kipindi chote cha miaka 8 tangu kuanzishwa kwake.

Monday, May 21, 2012

NIMEJIKUTA NIPO SALE NA MKWE LEO... HAH HAHH

Muda mwingine hutokea mkagongana kwenye mavazi yaani kukawa na mfanano yawezekana wa rangi za nguo zenu ama ikawa sale kabisaaa kwa kila kitu, hicho ndo kilichotokea leo. Bahati Alex (Mkwe yangu) alinitangulia kufika kwa job, baadae nami nikafika mweeh! Tukaishia kucheka tu na kila mmoja kumpa sifa zake mwenzake kuwa kapendeza, basi tukaona si dhambi japo kupata kumbukumbu mbili tatu na kuzitupia kiduchuni....Karibu mpendwa.
Kaa humo
Anko na jirani yangu pia Abdul akaona isiwe tabu nae ang'ae na Kiduchu japo kidogo mweeh!
Raha tupu
Mamaa ya JAMBO BEAT (Bahati Alex)

Ankooooo


KUTOKA MIGOLI MTERA, ZILINIVUTIA TU...Mtu na chama chake bana, bendera ya chama chako unaiweka popote unapo jisikia ili mradi pawe panapo kuhusu. Hapa ni Migoli Mtera kulikuwa na mkutano ulioendeshwa na wana chama wa CHADEMA wakishirikiana na wananchi wa Migoli kujadili kuhusu Katiba mpya.
Hawa ni marafiki zangu, nawapenda sana watoto maana ni marafiki wa kweli
Wee nani kakwambia njaa ina mwenyewe?
Hii picha niliipiga kwa mbaliii na kilichonivutia ni huyo dada upande wa kushoto alivyo chomeka chanuo kunako nywele, ni style ya zamani lakini vijijini bado wanaiendeleza sijajua kama alikuwa anataka akasuke ama ndo aliamua kuwa hivyo kwa siku hiyo. Pole mpendwa wangu picha haionekani vizuri.
Watoto bwana, ukikaa na kuwafuatilia kuanzia asubuhi mpaka jioni unaweza usiwaelewe lakini wenyewe waelewana kwa kila kitu wanachokifanya ama kuongea, mi huwa nafurahi tu na sifa na utukufu kumrudishia muumba, maana huu ni uweza wake.
Lady j dee hakukosea kutamani kuwa malaika aisee, hata mi naungana nae bana utoto raha asikwambie mtu... Kama hivi ukichafuka unaogeshwa kama bi dada Jesca hapa kwa raha zake

Bwan'kaka akipata ngoma baada ya ngoma, utamtaka sasa?

Friday, May 18, 2012

KILA MTU ANA MBINU ZAKE ZA USAKAJI MAHELA


Kila mtu analiwazo lake bana haswa pale anapokuwa na msongo wa mawazo, baba huyu anaekaa maeneo ya kitanzini Iringa Mjini ye liwazo lake ni hili gitaa lake, akishamaliza mishe zake za usakaji mshiko akili inakuwa imechoka kifaa pekee kinachoweza kufanya akawa sawa ni hili gitaa na analikung'uta haswaa, wanaoguswa na nikuno yake basi kumtunza hailipiwi... Mi pia ni mmoja wawalio pagawishwa nauchanaji nyuzi wake... Chukua hiyooo!!!

Wakati mzuka wa gitaa umepanda akaja mama muuza vibatari, baba huyu akamwuliza bei yake mama akasema 800, dingi huyu akasema ye anaweza kumuungisha kwa mia7, mama akasema hailipi, baba akasema ye hapo ndo anaposimamia. Kijana hapo pembeni ye alienda hapo kusikiliza nyuzi zinavyochanwa na mdingi huyu...
"Kweli babaangu siku hizi makopo ya kutengenezea vibatari hayapatikani kirahisi, kwa hiyo mia 7 hailipi chukua tu kwa 800 jamani" Mdingi akasimamia palepale kwa 700
Mwisho wa siku mama akamuuzia kwa 700
Kweli mwanaume anakula kwa jasho
Daah! Polesana kakaangu
Wauza ulanzi hawa walikuwa wanaonja kwanza ulanzi wao kabla ya kuufikisha sehemu husika...akha, raha jipe mwenyewe mwenzangu ukisubiri kupewa mbona utachachaa?!
Asikwambie mtu bwana kazi na dawa aisee, akina mama na babaz wako biz na uchambuzi wa njegere ili wateja wasipate tabu kwenye ubanjuz pembeni wapata kimiminika cha ulanzi...chukua hiyooo!!
"Sijaja kuuza sura Iringa nimekuja kusaka mahela"
"We ilete tu hata kama imeliwa na panya mi ntaipiga kiraka na itavalika tena"

Hapa genge, hapa kutengeneza majiko bora mlandi huibi cha mtu basi siku zinasonga tu...
Hapa nadhani godzilla angetafuta lakuchumpa asingekosa
Hii ndo kitanzini bana, kila mtu yupo na hekaheka zake kama hivi
Angalia kinachokufaa, toa pesa, beba halafu usepe
Wanunuzi kama kawa wakutosha
Ule mlima uliokuwa unauona kwa mbaali ndo huu upo ipogoro..

Thursday, May 17, 2012

FURAHI NA WADAU WENZIO

J-ree, Fatma & Ne-mo
Eliud...Jiraniiiii
Aggy & Kidy
Miss pelle & Mama john
Kija vipi kaka kwema? Karibu iringa bana...hah hah
Mkweeee, b moco ila huyo mwenzio sijampata vyema nikumbushe
Nimewapenda tu na si vinginevyo...
Emmo na wake Tausi wawauache
Mamaake na John (Neema Msafiri) na Ne-mo
Kiduchu na Kidy wangu mtuache, hah hah hahha... anavituko sana huyu ukikaa nae hata dkk5 lazima ucheke sana ni mchekeshaji asiye lazima kupaka masizi usoni ndo achekeshe
Dj Mubba
Dada Anna vipi mwenzetu unaechart nae hasomeki nini?
J-ree na mchizi wako mmetokelezea aisee
Wadau wangu majina yenu yamenitoka, ahsanteni kwa ushirikiano
Eddo bandugu, vipi hiyo mikono ipo tayari kwa kumlaki nani tena mwenzetu?
Mwee! Kiduchu & Ney hamjielewi...
We Hatya wewe, unamtakia nini mubba wa watu kwa mkao huo wajameni?
Duuh!! utanisaidia na wewe mwenzangu mi mgeni hapa mwee!
Hhah hah hah...sijawahi kulielewa kama ni pozi ama ndo mzuka wa picha, kaka waukweli aitwa Maleges huyu...
TAUSI, hapana chezea yeye kwenye uzungushaji wa nyonga awapo stejin haswaa pale ulindimapo mziki wa mwambao (Taarabu), utamtaka sasaa?!
 

Sample text

Sample Text