Social Icons

Pages

Monday, May 10, 2010

JAMANI PENDO UMENIFANANISHA MAMY....


Mzima Dada? Naamini hata MALARIA nayo imeondoka sasa.
Mie mwema na familia pia. Ni pilika tuuu za kusaka maisha zinazoninenepesha kinyumenyume (wengine wanaita kukonda).
Haya sasa.
Niliandika makala maalum kuhusu siku ya kinamama na kwa bahati mbaya sikupata muda wa kujibu maoni ya waliochangia. Wa kwanza kuhusisha post hiyo na wewe ni Da'Mkubwa MiJAH ambaye alisema mke wangu anafanana na wewe. Sasa akaja na ndugu mwingine aitwaye PENDO ambaye amesema na hapa ninanukuu "Mzee wa changamoto nikuite shemeji kwani mke wako Dada Agness nilisoma nae Siha Sec Hai-Moshi kama atakuwa ananikumbuka mara ya mwisho nilikutana nae Azania front alikuwa kwenye harusi moja hivi toka hapo sijamuona tena na ndio mara namuona hapa blog kwako. Shes polite,and kind very respective sisy nadhani yuko hivyo hivyo umepata mke...Mungu awabariki sanaa...Pendo."
Haya dadangu. Msake rafikiyo pendo. Mimi nitaweka anwani ya blog yako kwenye majibu yangu kwao ili akusake na ukiweza weka email yako pale muwasiliane. Nadhani anakusaka.
Just funny how people wanaweza kufananisha watu kiasi hiki. I hope siku moja hatakuwa ndani ya daladala mtu akaita "Aggie" na asigeuke halafu ukaja kuambiwa kuwa "SIKU HIZI UNANATA HATA UKIITWA HAUITIKI".
Hahahahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
Post yenye haya mambo ni hii hapa http://changamotoyetu.blogspot.com/2010/05/kwa-mama-yangu-mamaa-wangu-mama-wa.html

http://www.changamotoyetu.blogspot.com

2 comments:

  1. Jamani ina maana hukusoma Siha Sec?
    Hahahahaaaaaaaaaaaa. Haya basi naamini Ndg Pendo ataweza kusaka na kupata yule aliyesoma naye.

    ReplyDelete
  2. Nimempata huyo amsakaye.
    Asante kwa kunijibu na stay connected

    ReplyDelete

 

Sample text

Sample Text