Monday, May 17, 2010
NILIUPENDA SAAANA HUU MSHITUKIZO JANA,KAMA URUDIE TENA VILEE....
Jana tulikuwa na kijikikao chetu cha watu wa4 (poleni sitowambia kinahusu nini lakini wapenzi,samahanini katika hilo)
Ilikuwa iwe wa5 lakini bahati mbaya mwenzetu m1 anaumwa kwahiyo hatukufanikiwa kuwanae...(nakuombea upone haraka sisy Lau)
Mwanzo tulipanga kukifanyia ofisini tu, lakini ghafla mie na mamaa wa jambo beat ama mama kijacho (bahati alex) tulibaki hatuna lakuuliza baada yakuambia na ndugu austine na achileus "pandeni kwenye gari twendeni" bila hata kujua tunakoenda,tukajitoma garini na safari ikaanza...
Haya karibuni tusafiri kwa pamoja wapendwa wangu.
Ukiwa unashusha toka I town,ipogoro inakuwa yaonekana kihivi.
Kitonga ndogo (mlima wa ipogoro) matengenezo bado yanaendelea,ila wamefanikiwa kuweka barabara poa kwa asilimia kubwa.
Kazi nzuri kwakweli...
Inavyoonekana kwa sasa
Natamani kuishi kwenye huu mlima, naupenda sana hata sijui kwanini.
Ahsante bwan'dereva kwa mwendo wa taratibu hatuna haraka,tufikishe salama sie.
Hili ni jambo la kawaida kukutana nalo kwa sasa pande hizi, siunajua na upanuzi wa barabara umepamba moto huku?...so usiogope,tutafika tu.
Kuna kitu kitasimama soon
kipanya kimekula vichwa mpaka kimecheuwa,pande za ilula hapa.
ilula matengenezo ya barabara bado yanaendelea,kwahiyo vumilia kichuuuchu kula vumbi.
kazi inaendelea na siku si nyingi kitu kitakuwa mkeka
tumeshafika kitonga, twaingia humo ndani
tumefika salama,,,ahsante mungu...cheka kidogo bathiii
Bahati alinambia "kijacho anapiga jamanii?" nikawa namsihi asisumbue mamiii...ha aah ahah
Bahati na achi wakienda kutupia macho mto ruaha,ila nasikia kuna mamba ni balaa.. uzio unatakiwa ili kunusuru watoto na hata watu wazima ili siku lisije sikika jambo la hatari mahala hapa.
Mama kijacho (bahati alex) na mie
Piga msosi mwanawane maisha yenyewe yakowapi bwanaaa?
Baada ya msosi kazi ikaanza,kaka alianza kama utani vileee...
Bahati akapiga ukelele "mtumeee,teh teh teh we achiii"
Wala hakujari,yeye huyooo
"Niruke nisirukee" mie nae "rukaaa"
Mara akasema amekumbuka kitu,akarudi zilipo nguo zake "kumbe ninayo nyingine ndani? nitaogelea na ya ndani bwana hii nyingine wacha niiache itanisave baadae" hahaa haa ha,mara tukashangaa binadamu anachojoa hiyo naninii...mayoooo haa haa..
"hapa sasa swaaaaafi"
Raha ikaanza kama hivi...kwa raha zake kuleeee.
Mmmh! mwenzangu kuogelea ni wito mwenzangu lool,shughuri kama hiyo ntaiwezea wapi nie?
Kichwa na kiwiliwili cha binadamu vyote vimo majini....Bahati akapiga kelele eti "mamaaaa mi sitaki bwana" haa haa haa.
Austine na achi wakionyesha ujuzi...haah haa ha
Jamani huyu kaka nilimhurumia kweli kweli, maana alikuwa anaogopa maji utadhani sijui vipi yaani.
Maana alikuwa anapiga kelele zakuogopa mpaka huruma, nikamuuliza "kwani vipi kakaangu kupiga kelele huko?"
Akasema anapenda kuogelea ila anaogopa maana mwaka 2006 maji yalitaka kumtoa roho...haa ha ha,jamani pole mwayego lol!!
Haya kakaaa, mi nina la kuzunguza basi? Natizama tuuu...
Baadhi ya wanyange watakao wania taji la miss iringa trh 21 mwezi huu, tuliwakuta wakiponda raha pande hizi.
Baada ya kufurahia vyakutosha tukakaa kujadili mawili matatu kuhusiana na kitu tulichoenda kukifanya mbali na kubadilisha mazingira.
Kikao kikaahirishwa mpaka tarehe iliyopangwa na kagiza nako kakawa kameingia "jamaniee tuondokeni sasa wapendwa"
kuna kitu mama kijacho alisema ila sikumbuki ninini maana alikuwa anatoa maneno mengi ya kutunyoosha mbavu mpaka unapenda..
Mwemdo wa kwenda kwenye kiberiti chetu ili tuking'oe makwetu..
Mama KIJACHO jamani kwakuagiza? Mmmh!
Hapo alikuwa anasubiria bamia zake toka kwa muuza, maana njia nzima alikuwa anasema "kijacho ana hamu na bamia leoo,acha kabisa nikiziona lazima ninunue" haa hahaah ha...haya mama kakate hamu.
Aliyekwambia wanaume huwa hawawanunulii wake zao mambomambo ya kukamilisha madikodiko ya jikoni ni naniii???
Achileus na Austine waliwajibika katika hilo....aisee niliwapenda zaidi.
Safari ya kurudi I town ikaanza,ila kiukweli nilikifurahia saaana kijisafari hiki na naamini huu ni mwanzo tu...
Shukrani kwenu kaka Austine na Achileus.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Agness ahsante sana kwa taswira hii yaani nimejikuta nami nipo safarini naye. Umenikumbusha mengiiiiii
ReplyDeletekaribu saaana dadangu kipenz,
ReplyDelete