Sunday, April 4, 2010
NYASI ZITANG'OKA LEO SAMORA....
leo kuanzia mida ya saa 8 mchana mambo yatakuwa vizuri kunako uwanja wa samora,kutokana na burudani itakayo patikana uwanjani hapo toka wa wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya kama bi dada toka chama la tip top ZUHURA,NEMO na AWILO PETRO toka mbeya ambao watatoa burudani bila kusahau kabumbu la kung'oa nyasi toka timu ya EBONY FM na wanasalamu wa IRINGA SALAM CLUB. nimetoka uwanja wa samora sio mida kwenda kuangalia mambo ya maandalizi kuhusiana na bonanza la leo yanavyokwenda...nimependezwa na kila kinachoandaliwa hapo maana kina kwenda kama inavyo takiwa.
niko na fundi mitambo wa ebony fm ndugu ACHILEUS DESDEL ambae pia anasimamia maandalizi ya hilo jukwaa na kuhakiki kwamba kila kitu kinakuwa vyema.
watoto pia wamepewa nafasi nzuri ya kukutana na watoto wenzao leo, na ndo maana wamewekewa kitu kama hiki (bembea)
mie na golikipa wa timu ya ebony fm b-sly...nimemwambia ole wake afungishe magoli ndo atatujua si ni akina nani...ha ha ha. ntakupa matokeo mdau wangu mwisho wa siku.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment