Wednesday, March 31, 2010
KUNANI IPOGORO WAJAMENI?
hii ni stand ya bus na daladala ipogoro iringa,wafanya biashara na abilia wake wanalalama saana juu ya stand hii kuwa msimu wa mvua huwa ni shida sana kwao kutokana na matope na madimbwi ya maji kuwa ni usumbufu kwao...kazi kwenu wahusika.
washkaji zangu nao wakaomba niwang'arishe kupitia kiduchu,nkaona si kesi na ndo kama hivi....watoto wamenikumbusha mbali hawa lol! kwa hiyo style ya kuonyesha dole,mi nilidhani imepitwa na wakati kumbe imerudi tena?
binadamu wanaishi humo na maisha yanasonga.
ulishawahi kula chips vumbi weyeee?...ipogoro sehemu zinapopatikana ndo zakumwaga,jaribu halafu unambie.
hata mishkati yapatikana na chachandu pembeni ilimlad siku inakuwa imepita vyema..
kuanzisha jambo ni rahisi, lakini umaliziaji wake huwa ni kimbembe.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment