Kila mtu analiwazo lake bana haswa pale anapokuwa na msongo wa mawazo, baba huyu anaekaa maeneo ya kitanzini Iringa Mjini ye liwazo lake ni hili gitaa lake, akishamaliza mishe zake za usakaji mshiko akili inakuwa imechoka kifaa pekee kinachoweza kufanya akawa sawa ni hili gitaa na analikung'uta haswaa, wanaoguswa na nikuno yake basi kumtunza hailipiwi... Mi pia ni mmoja wawalio pagawishwa nauchanaji nyuzi wake... Chukua hiyooo!!!
Wakati mzuka wa gitaa umepanda akaja mama muuza vibatari, baba huyu akamwuliza bei yake mama akasema 800, dingi huyu akasema ye anaweza kumuungisha kwa mia7, mama akasema hailipi, baba akasema ye hapo ndo anaposimamia. Kijana hapo pembeni ye alienda hapo kusikiliza nyuzi zinavyochanwa na mdingi huyu...
"Kweli babaangu siku hizi makopo ya kutengenezea vibatari hayapatikani kirahisi, kwa hiyo mia 7 hailipi chukua tu kwa 800 jamani" Mdingi akasimamia palepale kwa 700
Wauza ulanzi hawa walikuwa wanaonja kwanza ulanzi wao kabla ya kuufikisha sehemu husika...akha, raha jipe mwenyewe mwenzangu ukisubiri kupewa mbona utachachaa?!
Ag, yaani leo umenitembeza Iringa nimefurahi kweli je unaweza kupiga picha hapo ilipokuwa zamani Milimani Motel?
ReplyDelete