Ni Wewe ni kampeni iliyozinduliwa na redio Ebony FM iliyoko Nyanda za juu kusini, ikiwalenga zaidi wananchi wa vijijini ambao miundo mbinu ya umeme bado haijawafikia kwakuwasaidia kwa kuwapa majokofu yasiyotumia umeme, unga wa ngano na nguo... Hii yote ikiwa na dhumuni kubwa la kurudisha fadhila kwa wasikilizaji wa redio Ebony FM kwa kipindi chote cha miaka 8 tangu kuanzishwa kwake.
Featured Posts
Wednesday, July 16, 2014
Monday, May 21, 2012
NIMEJIKUTA NIPO SALE NA MKWE LEO... HAH HAHH
Muda mwingine hutokea mkagongana kwenye mavazi yaani kukawa na mfanano yawezekana wa rangi za nguo zenu ama ikawa sale kabisaaa kwa kila kitu, hicho ndo kilichotokea leo. Bahati Alex (Mkwe yangu) alinitangulia kufika kwa job, baadae nami nikafika mweeh! Tukaishia kucheka tu na kila mmoja kumpa sifa zake mwenzake kuwa kapendeza, basi tukaona si dhambi japo kupata kumbukumbu mbili tatu na kuzitupia kiduchuni....Karibu mpendwa.
KUTOKA MIGOLI MTERA, ZILINIVUTIA TU...
Mtu na chama chake bana, bendera ya chama chako unaiweka popote unapo jisikia ili mradi pawe panapo kuhusu. Hapa ni Migoli Mtera kulikuwa na mkutano ulioendeshwa na wana chama wa CHADEMA wakishirikiana na wananchi wa Migoli kujadili kuhusu Katiba mpya.
Hii picha niliipiga kwa mbaliii na kilichonivutia ni huyo dada upande wa kushoto alivyo chomeka chanuo kunako nywele, ni style ya zamani lakini vijijini bado wanaiendeleza sijajua kama alikuwa anataka akasuke ama ndo aliamua kuwa hivyo kwa siku hiyo. Pole mpendwa wangu picha haionekani vizuri.
Watoto bwana, ukikaa na kuwafuatilia kuanzia asubuhi mpaka jioni unaweza usiwaelewe lakini wenyewe waelewana kwa kila kitu wanachokifanya ama kuongea, mi huwa nafurahi tu na sifa na utukufu kumrudishia muumba, maana huu ni uweza wake.
Friday, May 18, 2012
KILA MTU ANA MBINU ZAKE ZA USAKAJI MAHELA
Kila mtu analiwazo lake bana haswa pale anapokuwa na msongo wa mawazo, baba huyu anaekaa maeneo ya kitanzini Iringa Mjini ye liwazo lake ni hili gitaa lake, akishamaliza mishe zake za usakaji mshiko akili inakuwa imechoka kifaa pekee kinachoweza kufanya akawa sawa ni hili gitaa na analikung'uta haswaa, wanaoguswa na nikuno yake basi kumtunza hailipiwi... Mi pia ni mmoja wawalio pagawishwa nauchanaji nyuzi wake... Chukua hiyooo!!!
Wakati mzuka wa gitaa umepanda akaja mama muuza vibatari, baba huyu akamwuliza bei yake mama akasema 800, dingi huyu akasema ye anaweza kumuungisha kwa mia7, mama akasema hailipi, baba akasema ye hapo ndo anaposimamia. Kijana hapo pembeni ye alienda hapo kusikiliza nyuzi zinavyochanwa na mdingi huyu...
"Kweli babaangu siku hizi makopo ya kutengenezea vibatari hayapatikani kirahisi, kwa hiyo mia 7 hailipi chukua tu kwa 800 jamani" Mdingi akasimamia palepale kwa 700
Wauza ulanzi hawa walikuwa wanaonja kwanza ulanzi wao kabla ya kuufikisha sehemu husika...akha, raha jipe mwenyewe mwenzangu ukisubiri kupewa mbona utachachaa?!
Thursday, May 17, 2012
FURAHI NA WADAU WENZIO
Subscribe to:
Posts (Atom)